Hatutaahirisha mitihani ya kitaifa-Waziri Magoha asema

Muhtasari
  • Isitoshe aligusia mambo na uteketezaji  wa shule ambao umekuwa ukiendelea katika maeneo tofauti  nchini
  • Nakueleza kwamba  kitambo mtoto alikuwa wa jamii  lakini wakati huu mambo ni tofauti ambapo mtoto anatunzwa bila kurekebishwa
CS magoha
CS magoha

Waziri wa elimu George Magoha  Ijumaa  akiwa katika chuo kikuu cha  Kabarak aliwaambia wanafunzi ambao wanajiadaa kukalia mtihani wa kitaifa  wa shule ya msingi na ule wa kidato cha nne kwamba mtihani utaendelea kama ilivyopangwa na wizara ya elimu.

Magoha ambaye alikuwa  anahotubia wanafunzi wa chuo cha KabaraK ambao walihitimu mwaka huu alitoa dukuduku ambao wanafunzi waliokuwa nao ya mtihani kuharishwa

“ Nataka kutangaza kuwa mtihani uko tayari  na utakuwa wa  machi... hatutabadilisha kalenda ya mtihani “ alisema Magoha

Isitoshe aligusia mambo na uteketezaji  wa shule ambao umekuwa ukiendelea katika maeneo tofauti  nchini.

Nakueleza kwamba  kitambo mtoto alikuwa wa jamii  lakini wakati huu mambo ni tofauti ambapo mtoto anatunzwa bila kurekebishwa

“Wakati wa kitambo watoto walikuwa  wa jamii kwa sasa tunaelekea kwa Sodom na Gomorrah  mahali ambapo wazazi wanatunza watoto wao kama yai. Tunacho kwa sasa ni watu wakubwa  ambao wanaitwa watoto kwa sababu wako shule”