In Summary

•Maafisa wa DCI wamesema ingawa wawili hao walilfanikiwa kutoroka, kamera za kukagua usalama zilizo kwa transfoma hizo tayari zilikuwa zimechukua picha zao na kuzituma kituoni

Image: TWITTER DCI

Wapelelezi katika kaunti ya Makueni wanawasaka wezi wawili ambao walioharibu transforma za umeme katika kituo cha SGR  cha Makindu.

Wezi hao wawili waliokuwa wamejihami kwa spana walinaswa na kamera za CCTV usiku wa Ijumaa wakiharibu transfoma ambazo husambaza umeme katika kituo hicho.

Maafisa kutoka vituo vya  polisi vya Makindu na Emali walipofika katika eneo la tukio kuwakamata, washukiwa walitimua mbio na kutoweka katika kichaka kilicho karibu baada ya kuona  taa za gari la polisi lililokuwa linaelekea upande wao kwa kasi.

Maafisa wa DCI wamesema ingawa wawili hao walilfanikiwa kutoroka, kamera za kukagua usalama zilizo kwa transfoma hizo tayari zilikuwa zimechukua picha zao na kuzituma kituoni.

Kufuatia hayo umma umeonywa dhidi ya kuharibu miundombinu ya kitaifa kama vile reli kwani mtu huenda akashtakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi na Ugaidi.

View Comments