Mamlaka ya Keli ya Kenya
Image: Image: picha:twitter /Hisani

Shirika la reli siku ya jumapili lilitangaza safari za treni  kurejelewa baada ya kusitishwa kwa takribani siku 6.

Kupitia mtandao wa twitter Shirika hilo  limesema huduma katika njia ya Nairobi- Madaraka-Pipeline-   Embakasi  pamoja na  zinazopitia njia ya Nairobi- Kisumu-Limuru zitarejea kuanzia Jumatatu, Januari 3, 2022

"Tafadhali kumbukeni kuwa operesheni ya kawaida inaanza tena kesho, Januari, 3 kulingana na ratiba  ya kawaida iliyotolewa" shirika hilo lilinakiri kwa mtandao wake.

Shirika la Reli la Kenya lilipunguza huduma hizo sa usafiri wa Treni, mnamo Desemba 28, 2021  kufuatia idadi ndogo ya abiria iliyojitokeza wakati wa msimu wa sherehe za Krismasi na mwaka mpya. Mahitaji ya usafiri wa Treni yameanza kuongezeka  huku abiria wengi wakionekana kujitokeza.

Isitoshe Shirika hilo liliwahakikishia abiria kuwa nitaendelea kuwa hudumia kwa bei nafuu na ufanisi wa hali ya juu.

"Tunajitahidi kutoa salama, ufanisi wa kuaminika na kwa bei nafuu"

View Comments