In Summary

• Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria amesema kwamba chama chake kipo katika mazungumzo ya kuunda muungano na mrengo wa Kenya Kwanza unaoongozwa na naibu rais William Ruto.

• Kuria amesema kwamba chama chake kitatoa taarifa zaid kuhusu uamuzi huo.

 

Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Image: MAKTABA

Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria amesema kwamba chama chake kipo katika mazungumzo ya kuunda muungano na mrengo wa Kenya Kwanza unaoongozwa na naibu rais William Ruto.

Kulingana na Kuria, Chama Cha Kazi kwa ushirikiano na vyama vingine 21 vimeanza mazungumzo na vuguvugu la Kenya Kwanza ili kuuunda muungano thabiti ambao utazingatia kuleta amani na kuboresha maisha ya wakenya.

Kuria amesema kwamba chama chake kitatoa taarifa zaidi kuhusu uamuzi huo.

Ikumbukwe kwamba siku chache zilizopita,Kuria alikuwa amesema kwamba yuko tayari kushirikiana na muungano wa OKA iwapo hawataingia katika makubaliano na Azimio.

Mbunge huyo awali akijibu kuhusu mrengo ambao angependa kujihusisha nao, alisema kwamba angependa kushirikiana na viongozi ambao wana azma ya kubadilisha maisha ya wakenya wa kawaida.

Moses Kuria alitangaza kwamba atakuwa anawania kiti cha ugavana katika kaunti ya Kiambu.

View Comments