In Summary

• Kinara wa chama cha ODM Raila ndiye ndiye mgombea wa kiti cha urais nanayependelewa zaidi katika kaunti ya Nairobi, hii ni kulingana na ripoti ya Tifa.

• “Huku Raila Odinga akiwa kiongozi anayependekezwa na wengi katika kaunti ya Nairobi, pengo kati yake na Ruto si kubwa ikiashiria kwamba kutashuhudiwa kivumbi kikali katika eneo hilo,” Tifa ilisema.

KInara wa ODM Raila Odinga
Image: George Owiti

Kinara wa chama cha ODM Raila ndiye ndiye mgombea wa kiti cha urais nanayependelewa zaidi katika kaunti ya Nairobi, hii ni kulingana na ripoti ya Tifa.

Kulingana na kura hizo za maoni zilizotangazwa rasmi Alhamisi, Raila anaendelea kuwa maarufu katika kaunti ya Nairobi kwa asilimia 41.

Anafuatwa kwa karibu na naibu rais William Ruto ambaye anamiliki asilimia 31.

“Huku Raila Odinga akiwa kiongozi anayependekezwa na wengi katika kaunti ya Nairobi, pengo kati yake na Ruto si kubwa ikiashiria kwamba kutashuhudiwa kivumbi kikali katika eneo hilo,” Tifa ilisema.

Katika kura hizo, seneta Johnson Sakaja anaonekana kuwa na nafasi ya juu zaidi kuibuka kidedea kwenye  kinyang’anyiro cha ugavana katika uchaguzi wa Agosti 9.

Sakaja anaongoza kwa asilimia 23, Tim Wanyonyi ni wa pili na asilimia 14 huku Ann Kananu akifunga orodha hiyo kwa asilimia 7. Hata hivyo, asilimia 23 ya wakazi wa Nairobi bado hawajafanya uamuzi kuhusu nani watakayemchagua.

 Asilimia kubwa ya waliohusika katika kura hiyo ya maoni wanaonekana kutoamua kuhusu chaguo lao katika kinyang’anyiro cha useneta huku baadhi yao wakipendekeza Sakaja aendelee kushikilia nafasi hiyo.

Esther Passaris anazidi nkuongoza katika umaarufu kwenye kivumbi cha uwakilishi nkina mama kwa asilimia 34, Millicent Omanga akiwa mpinzani wake wa karibu na asilimia 9.

 

 

View Comments