In Summary

• Wazee hao wameomba msamaha kwa Raila Odinga kufuatia kitendo cha ndege ya Raila kupigwa mawe.

• Wataandaa hafla ya kutakasa eneo hilo baada ya siku 40 kulingana na tamaduni za jamii hiyo.

Wazee wa jamii ya Kalenjin hatimaye wametoa tamko lao kuhusu kisa cha ndege ya kinara wa ODM Raila Odinga kupigwa mawe.

Baraza hilo la wazee almaarufu Muyot lilisema kwamba kwamba litaandaa hafla ya kutakasa eneo la tukio hilo, baada ya siku 40 kulingana na tamaduni za jamii hiyo.

Wakizungumza na wanahabari siku ya Jumatano, wazee hao walimuomba Raila Odinga msamaha huku wakikashifu vikali kitendo hicho na wale wote waliohusika.

Wakiongozwa na Paul Tumbo miongoni mwa wengine, walisema kwamba kila Mkenya ana ruhusa ya kuuza sera zake katika sehemu yoyote nchini.

"Mzee Raila Odinga ni kiongozi wa heshima, tunaomba msamaha kwa niaba ya jamii ya Kalenjin," wazee hao walisema.

Kisa cha ndege ya Raila Odinga kupigwa mawe kilifanyika karibu wiki moja iliyopita katika mazishi ya mfanyibiashara Jackson Kibor.

Kitendo hicho kilipelekea kutupiana cheche kati ya viongozi wanaoegemea upande wa Raila Odinga na ule wa naibu rais William Ruto.

View Comments