In Summary

• Katiba institute na LSK wapeleka kesi mahakamani kupinga hatua ya Safaricom kupata picha za wateja wao katika shughuli ya usajili wa sim card.

• Taasisi hizo zilidai kwamba hatua hiyo ni kinyume cha sheria.

Umati katika duka la Safaricom ukisubiri kuhudumiwa.
Image: SHARON MAOMBO

Katiba Instute  na LSK zimewasilisha kesi kortini kupinga uamuzi wa Safaricom kupata picha au data za  kibayometriki za kama sharti la usajili wa Sim card.

Kupitia mawakili Dudley Ochiel na Wanjeri Wangui, makundi ya washawishi yanahoji kuwa kupiga picha za waliojisajili ni kinyume cha sheria na ni kinyume cha Kanuni za Taarifa na Mawasiliano za Kenya (Usajili wa SIM card) 2015, na pia kifungu cha 31 cha Sheria ya Kulinda Data, 2019.

"Na zaidi kukomesha tishio la Safaricom la kuzima wateja ambao wamesajiliwa na kuthibitishwa kwenye mfumo wa kawaida *106#," nyaraka za mahakama zilisema.

Wanasema kuwa mnamo Aprili 10, CA ilifafanua kuwa Kanuni za Taarifa na Mawasiliano za Kenya (Usajili wa SIM-kadi), 2015 zinazosimamia usajili na uthibitishaji wa waliojisajili "hazihitaji watumiaji kuwasilisha picha zao wakati wa kujiandikisha."

Ikumbukwe kwamba CA iliongeza muda hadi Oktoba 15 kwa wateja wote kusajili sim card zao, la sivyo huduma zao zitakatishwa.

Hatua hii ilijiri baada ya kelele za wakenya katika mitandao ya kijamii wakisema kwamba mchakato huo ulikuwa umeharakishwa.

View Comments