Spika wa bunge la Kaunti ya Nairobi Benson Mutura ameagizwa kufika katika afisi za Kurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) kwa madai ya wizi.
Anatarajiwa kufika katika afisi za DCI mwendo saa mbili usiku ili kuangazia madai ya wizi. "Nachunguza kuhusu madai ... ya wizi.
Nina sababu za kuamini kuwa wewe, Benson Mutura unahusishwa na kosa hilo au una taarifa ambazo zinaweza kusaidia katika uchunguzi," agizo hilo lilieleza.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake Jumatano, Mutura alisema polisi walijaribu kumkamata katika afisi zake asubuhi. Alitaja jaribio hilo la kukamatwa kama hujuma kwa sababu alitangaza kwamba ataunga mkono azma ya urais ya Naibu Rais William Ruto.
"Leo asubuhi nikiwa afisini, afisa fulani alikuja kunikamata bila agizo la kufanya hivyo.
Walichokifanya ni kinyume kabisa na kanuni za Kaunti ya Nairobi," alisema. Alisema mara moja alifungwa pingu baada ya kupinga hatua ya maafisa hao.
"Niko tayari kutii wito. Nimekuwa na uazi katika kile nimekuwa nikifanya," alisema.