In Summary

•Inadaiwa kwamba Muruthi alikuwa mkuu wa magenge wahalifu walikuwa maeneo tofauti kama vile mtaa wa Mathare, Huruma na Pangani.

Mshukiwa mkuu wa magenge wahalifu
Image: DCI

Maafisa wa upelelezi wa DCI Starehe, walifaulu katika juhudi zao  za upelelezi na kumua jambazi mashuhuri ambaye alikuwa mkuu wa genge la Ruai, lililohusika na ongezeko la mashambulizi ya silaha ndani ya Ruai na viunga vyake.

Paul Muriithi Naomi almaarufu Muruthi, ambaye amekuwa kwenye rada za wapelelezi kwa muda wa miezi michache iliyopita alijeruhiwa vibaya kwa risasi, baada ya kukaidi amri ya kujisalimisha.

Maafisa hao wa upelelezi ambao walipata  habari kuhusu makao ya mshukiwa, walimtafuta hadi kwenye nyumba yake ya kukodi iliyoko Githunguri, Ruai, viungani mwa jiji.

Inadaiwa kwamba Muruthi alikuwa mkuu wa magenge wahalifu walikuwa maeneo tofauti kama vile mtaa wa Mathare, Huruma na Pangani.

Wakati wapelelezi walifanikiwa kufika kwake nyumbani na kujitambulisha, Muruthi aliwajibu kwa kufyatua risasi kupitia kwa dirisha yake, Wapelelezi hoa pia walijibu kwa kufyatua risasi pia na kufanikiwa kumua.

Walimpata na Bastola ya Ceska yenye nambari B 681256 iliyokuwa na risasi nne za 9mm ilipatikana, huku katriji 11 zilizotumika zikiwa zimetapakaa eneo la tukio.

Baada ya uchunguzi wa awali, ilibainika kuwa bunduki hiyo ilikuwa imeibiwa kwa nguvu kutoka kwa mtu aliyekuwa na bunduki ya kiraia wiki moja iliyopita.

Wakati wa tukio hilo baya, raia huyo alipoteza thamani ya zaidi ya shilingi  nusu milioni.

Mwili wa mhalifu huyo ulihamishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha jiji.

 

View Comments