In Summary

• Kenya Kwanza ilielezea imani ya kutatua vizingiti vyote ili kuafikiana na wenzao wa Azimio.

Menyekiti mwenza wa mazungumzo ya pamoja George Murugara

Upande wa Kenya Kwanza katika mazungumzo ya pamoja ya pande mbili umeshutumu wenzao wa Azimio kwa kuweka vizuizi visivyo vya maana katika juhudi za kufanyika kwa mazungumzo. 

Upande wa Kenya Kwanza ukiongozwa na mwenyekiti George Murugara umedai kuwa Azimio wanatafuta visingizio vya kuvuruga mazungumzo hayo. Murugara alisema kwamba kila mmoja katika mazungumzo hayo anafaa kujiona kiwango sawa na wengine na kwamba hakuna aliyejuu kuliko mwingine.

Hata hivyo alielezea imani ya kutatua vizingiti vyote ili kuafikiana na wenzao wa Azimio.   Murugara alisema kuna masuala ya dharura kama vile tume Huru ya mipaka ya uchaguzi ambayo hayawezi kuzuiwa kwa muda mrefu sana. 

"Tunahitaji kuzungumza na kukubaliana, tunahitaji kujua kutoka kwao ni nini suala la sheria ya sasa, ili tukubaliane juu ya njia ya mbele, na ikiwa ni lazima tubadilishe sheria, tunaileta kwenye bunge." Murugara alisema. 

Murugara alisema atamwandikia mwenyekiti mwenza Otiende Amollo ambaye alimshutumu kwa kusimamisha mazungumzo kabla ya wakati wake. Murugara anasema atamwomba mwenyekiti mwenza kufanya mazungumzo ili kusuluhisha maswala ambayo hayajakamilika kabla ya kurejelea mazungumzo kabla ya makataa ya Azimio Jumanne.


View Comments