In Summary

• Kikao kilifanyika bila kuripotiwa na vyombo vya habari kama ilivyokuwa desturi katika mikutano ya awali.

•Haieleweki kama wabunge walikuwa na idadi kamili ya kutosha kulingana na katiba ya nchi inayohitaji wabunge 50 katika Bunge la Kitaifa.

•Maswali pia yameibuka kuhusu kwa nini kupelekwa kwa majeshi kulitangazwa rasmi kabla ya kupitishwa na Bunge.

Mbunge Otiende Amollo
Image: Facebook

Bunge la Kitaifa limeidhinisha kupelekwa kwa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF) kusaidia polisi katika maandamano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya Mswada wa Fedha wa 2024.

Idhini hiyo imefanyika Jumatano wakati wa kikao maalum na imezua utata kuhusu msingi wake kisheria na jinsi ilivyofanyika.

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo alitumia mitandao ya kijamii kueleza kwamba kikao kilifanyika bila kuripotiwa na vyombo vya habari kama ilivyokuwa desturi katika mikutano ya awali.

Pia haieleweki kama wabunge walikuwa na idadi kamili ya kutosha kulingana na katiba ya nchi inayohitaji wabunge 50 katika Bunge la Kitaifa.

Amollo alidai kwamba katika dakika 30, Bunge lilipitisha kwa kauli moja kupeleka jeshi kabla ya kuvunja kikao kwa mapumziko.

Katiba inaagiza serikali kutafuta idhini ya Bunge la Kitaifa kabla ya kupeleka majeshi mahali popote.

 "Na, bila vyombo vya habari, bila wabunge wengi, bila mjadala sahihi, ndani ya dakika 30, bunge la kitaifa limefanya Kenya kuwa nchi ya kijeshi; Kuweka KDF bila kueleza mahali, kwa nini au kwa muda gani na walifanya hivyo kinyume na kipengee 241(3)(c). Mungu Atubariki," Amollo alisema kwenye jukwaa lake la X.

Zaidi na hayo, wakosoaji wameibua wasiwasi kuhusu jinsi wabunge wanavyoweza kukutana bila chombo cha kufananisha mamlaka na hadhi ya Bunge

Maswali pia yameibuka kuhusu kwa nini kupelekwa kwa majeshi kulitangazwa rasmi kabla ya kupitishwa na Bunge.

Wabunge sasa wanatarajiwa kuvunja kikao kwa mapumziko Jumatano na kuanza vikao vya kawaida Jumanne, Julai 23.

Jumanne, wabunge walipitisha Mswada wa Fedha wa 2024 pamoja na marekebisho yake. Pia walipitisha Mswada wa Matumizi ya Fedha wa 2024 ambao ulipitishwa na kamati nzima ya Bunge.

Baada ya maandamano, picha zilisambazwa mtandaoni Jumatano asubuhi za maafisa wa KDF waliowekwa kulinda miundo mbinu ya serikali.

View Comments