Timu ya  taifa  ya voli boli ya wanawake Malkia Strikers ilifuzu kwa michuano ya Olimpiki baada ya kuillaza Nigeria seti 3-0 jana nchini Cameroon katika kinyang'anyiro cha kufuzuzu barani Afrika.

Malkia stirkers walishinda kwa seti za  25 -15 , 25- 21 na 25-12, na kumaliza mbele ya wenyeji Cameroon ambao walimaliza wa pili. Kenya imefuzu kwa michezo ya Japan mwaka 2020 na wanarejea chini ya kocha mkuu Paul Bitok baada ya miaka 15.

Ndoto ya waogeleaji wa Kenya kushiriki katika michezo ya Olimpiki huenda isitimie baada ya  shirikisho la uogeleaji nchini FINA kuipiga marufuku shiriskiho la uogeleaji la  Kenya.

Marufuku hiyo inatokana na ukosefu wa ofisi iliyo imara, baada ya kukosa kufanya uchaguzi  tangu mwaka wa 2014.  Kulingana na sheria za Fina,   wanachama wote wanahitajika kufanya uchaguzi angalau baada ya miaka miwili jambo ambalo Kenya haijatimiza.

Agenti wa  Gareth Bale anasema mchezaji huyo hataondoka  Real Madrid katika kipindi cha uhamisho wa Januari wala mwishoni mwa msimu. Kocha wa  Madrid  Zinedine Zidane alijaribu kumuuza Bale  mwanzoni mwa msimu huku akidai hayuko katika mipango yake, lakini alibadili nia  na kumweka katika timu ya kwanza. Bale  ana mkataba hadi msimu wa mwaka 2022 na  ni  vilabu chache  ambavyo vinaweza  kumlipa kwani anapata pauni laki 6 kama marupurupu.

Kiungo wa zamani wa kimataifa   wa Kenya  Peter “Pinchez” Opiyo amejiunga na timu ya daraja la pili  Nairobi City Stars. Pinchez ambaye anaondoka  kutoka klabu ya Finland  SJK  hapo awali alichezea Gor Mahia, Tusker na Afc Leopards, ameandikisha mkataba wa miezi  18  na vijana hao wa Kawangware. Afisa mkuu mtendaji wa Stars  Patrick Korir  anadai Pinchez ataongeza udhabiti katika  kikosi hicho.

Manchester United imekubali kuwa haitafanikiwa kumleta Old Trafford kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 27. Wakati huo huo Tottenham Wameafikia mkataba wa pauni milioni 28 kumnunua mshambulizi wa AC Milan na Poland Krzysztof Piontek mwenye umri wa miaka   24

Kocha wa Gor Mahia Steven Polack alituzwa  kwa kuwa kocha bora wa ligi ya KPL mwezi Novemba, na kunyakua taji hilo kwa mara ya pili mfululizo   baada ya kunyakua lile la mwezi Oktoba.  Mzaliwa huyo wa Uingereza alishinda mechi tatu mtawalia na  kujizolea alama tisa, zaidi ya makocha wenzake Robert Matano wa Tusker, Zedekaih Otieno wa KCB . Alitunukiwa shilingi  elfu 75.

Kwingineko Kiungo wa Manchester United Ashley Young amekataa mkataba mpya wa mwaka mmoja, huku akiaminiwa kutaka kuondoka Old Trafford katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi huu.

Mzaliwa huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 34 amesalia na miezi sita katika kandarasi yake na amekua akihusishwa na klabu ya Italia Inter Milan.  Hata hivyo kocha mkuu Ole Gunnar Solskjaer anataka asalie United  kwani ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa  ambaye  anaweza kucheza kama mlinzi.

View Comments