Daniel Ricciardo kujiunga na timu ya McLaren msimu mpya wa Formula one 2021
Daniel Ricciardo anatarajiwa kujiunga na timu ya Mclaren inayoshiriki katika michezo ya Formula One akichukua nafasi iliyoachwa na Carlos Sainz aliyejiunga na Ferrari.
Mabadiliko hayo yametangazwa na wasimamizi wa kampuni hizo kama njia ya maandalizi kwa msimu mpya wa Formula One.
Ricciardo atashirikiana na Briton Lando Norris, huku Sainz akitarajiwa kurithi mikoba iliyaochwa na bingwa mara nne wa mashindano hayo Sebastian Vettel aliyetangaza mapema wiki jana kuwa ataondoka kwa timu ya Ferrari msimu huu utakapomalizika.
Mkuu wa McLaren Zak Brownamesema Ricciardo ataleta mabadiliko makubwa katika timu hiyo japo akasema Sainz alikuwa ameafikia viwango vikubwa.
Naye mkuu wa kampuni ya Ferrari Mattia Binotto aliongezea kuwa Sainz yuko na kila kitu kinachomfanya kujiunga na timu hiyo.
"had proved to be very talented and has sown that he has the technical ability and the right attributes". amesema Binotto
Vettel alitangaza kuwa ataondoka kwenye kikundi cha Ferrari baada ya msimu kumalizika.