In Summary

•Mechi za Jumapili kuamua ni klabu zipi zitasalia kwenye nne bora kati ya Chelsea, Liverpool na Leicester

•Klabu moja kati ya Tottenham, Arsenal na Everton ndiyo itahitimu kuingia kwenye Europa Conference League

kikombe cha epl
Image: Hisani

Ligi kuu ya Uingereza inatarajiwa kukamilika siku ya Jumapili huku michuano kumi ya kuamua nani atakuwa wapi ikipigwa.

Ingawa mabingwa wa ligi hiyo na watakaoshukishwa ngazi washapatikana, pambano la kuhitimu kuingia ligi ya mabingwa(Champions League) na ligi ya Europa bado haijaamuliwa.

Klabu ya Manchester City inayoongozwa na Pep Guardiola iliweza kutwaa taji hilo kwa mara yake ya tano huku Fulham, Westbrom na Sheffield United zikizama hadi kwenye ligi ya Championship.
jedwali
Image: Hisani

Pambano la Jumapili litaangaziwa sana kuona nani kati ya Chelsea, Liverpool na Leicester atabakia kwenye nne bora huku klabu hizo zikiwa na pointi 67, 66, 66 mtawalia. Chelsea itakuwa inamenyana na Aston Villa, Liverpool ipambane na Crystal Palace nayo Leicester ikabiliane na Tottenham.

Klabu ya Manchester United ishajihifadhia nafasi kwenye ligi ya mabingwa huku ikiwa na alama 71 na mchuano mmoja wa kucheza. Itakuwa mgeni wa Wolves kwenye mechi ya mwisho.

Klabu ya Arsenal itakuwa inaomba sana ishinde Brighton nazo Tottenham na Everton zipoteze mechi zao ili kuweza kufufua matumaini yake ya kucheza Europa msimu ujao. Kwa sasa klabu hiyo imekalia nambari tisa na alama 58 huku Tottenham na Everton zikiwa na alama 59 kila mmoja zikichukua nambari 7 na 8 mtawalia.

View Comments