In Summary

•Ndoto za bingwa wa kutupa mkuki Julius Yego kuongeza medali nyingine kwenye kabati lake zilififia mapema asubuhi ya Jumatano baada yake kushindwa kufikisha alama zilizohitajika kuhitimu kuingia fainali.

•Yego ambaye alijinyakulia fedha kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Rio De Janeiro, Brazil mwaka wa 2016 amekuwa na msimumbaya  uliosheheniwa na majeraha.

Mwanariadha Julius Yego
Image: HISANI

Nchi ya Kenya imeendelea kupokea matokeo hafifu kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea jijini Tokyo Japan huku mabingwa waliotiliwa imani kubwa wakionekana kulemewa.

Ndoto za bingwa wa kutupa mkuki Julius Yego kuongeza medali nyingine kwenye kabati lake zilififia mapema asubuhi ya Jumatano baada yake kushindwa kufikisha alama zilizohitajika kuhitimu kuingia fainali.

Yego almaarufu kama 'YouTube Man' alimaliza katika nafasi ya 24 baada yake kurusha mkuki umbali wa mita 77.34 chini ya alama iliyohitajika ya umbali wa 83.50.

Hata hivyo, alama alizoandikisha  mwanariadha huyo katika uwanja wa Olimpiki mida ya saa kumi unusu asubuhi ndizo alama zake  bora msimu huu.

Yego ambaye alijinyakulia fedha kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Rio De Janeiro, Brazil mwaka wa 2016 amekuwa na msimumbaya  uliosheheniwa na majeraha.

View Comments