In Summary

 

  •  Lampard aonyeshwa mlango  baada ya miezi 18 usukani 
  • The blues hata hivyo imejipata pabaya katika ligi ya premier baada ya kushindwa katika mechi za  nane zilizopita .
Frank Lampard

 Chelsea imemfuta kazi kocha Frank Lampard baada ya kuwa hatamuni kwa miezi 18 .

 Lampard ,mwenye umri wa miaka 42 awali alikuwa  kiungo wa kati katika kilabu hiyo  na anaiacha  Chelsea katika nafasi ya 9 kwenye jedwali la ligi ya premia  baada ya kushindwa wiki jana na  Leicester City na wameshinda mchuano mmoja pekee  katika mechi tano za ligi  . Mchuano wake wa mwisho  ulikuwa siku ya jumapili katika kombe la FA  raundi ya nne ambapo waliishinda  Luton mabao matatu kwa moja .

Lampard  aliteuliwa kocha wa The Blues kwa mkataba wa  miaka mitatu  alipochukua nafasi hiyo kutoka kwa  Maurizio Sarri  julai mwaka wa 2019

 Aliwaongoza  kumaliza katika nafasi ya nne katika fainali ya kombe la FA   katika kipindi chake cha kwanza usukani  . The blues hata hivyo imejipata pabaya katika ligi ya premier baada ya kushindwa katika mechi za  nane zilizopita .

 

View Comments