In Summary

•Mechi za kuhitimu kuingia robo fainali zilikamilika usiku wa Jumanne kwa kishindo huku mechi mbili kubwa zikichezwa.

•Mshambulizi matata wa klabu ya Tottenham, Harry Kane aliendelea kuangamiza ndoto za Ujerumani kwa kufunga bao maridadi katika dakika ya 86 na kuwatimua nje ya kombe hilo.

•Mechi nyingine iliyochezwa usiku wa Jumanne ni kati ya Uswidi na Ukraine.  Ukraine waliweza kufuzu kuingia robo fainali baada ya kuwapiga Uswidi 2-1.

Harry Kane akisherehekea bao dhidi ya Ujerumani
Image: Hisani

Michuano ya EURO 2020 imeendelea kusisimua na kushangaza wapenzi wa kandanda wengi kote ulimwenguni huku tukikaribia kujua taifa lipi lititwaa ushindi wa kombe hilo.

Mechi za kuhitimu kuingia robo fainali zilikamilika usiku wa Jumanne kwa kishindo huku mechi mbili kubwa zikichezwa.

Mechi ambayo ilikuwa imesubiriwa kwa hamu ni kati ya Three Lions ya Uingereza na Ujerumani. Timu hizo mbili zimekuwa zikipigiwa debe kushinda taji hilo mwaka huu.

Hata hivyo, mabao mawili ya Uingereza kwenye kipindi cha robo ya mwisho yalitosha kubandua mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa 2014.

Mlinzi wa Manchester United, Luke Shaw alimsaidia mshambulizi wa Manchester City, Raheem Sterling kuifungia Uingereza bao la kwanza katika dakika ya 75.

Mshambulizi matata wa klabu ya Tottenham, Harry Kane aliendelea kuangamiza ndoto za Ujerumani kwa kufunga bao maridadi katika dakika ya 86 na kuwatimua nje ya kombe hilo.

Mechi nyingine iliyochezwa usiku wa Jumanne ni kati ya Uswidi na Ukraine.  Ukraine waliweza kufuzu kuingia robo fainali baada ya kuwapiga Uswidi 2-1.

Mlinzi wa klabu ya Manchester City, Oleksandr Zichenko alifungia Ukraine kwenye dakika ya 27 kabla ya Emil Forsberg kusawazishia Uswidi katika dakika ya 43. Dakika 90 za kawaida ziliisha mechi hiyo ikiwa sare ya 1-1 na kufanya mechi iende hadi dakika za ziada.

Bao la Artem Dovbyk katika dakika ya 121 lilipatia Ukraine ushindi na kuwasaidia kuingia robo fainali.

Katika mkondo wa robo fainali, Uswisi itakabiliana na Uhispania siku ya Ijumaa mwendo wa saa moja usiku kabla ya Ubelgiji kumenyana na Italia saa nne usiku huo.

Ucheki watapambana na Denmark Jumamosi saa moja usiku kisha Ukraine wapatane na Uingereza saa nne usiku huo.

Baadae kombe hilo litaingia mkondo wa semi fainali.

View Comments