In Summary

• Matumaini ya klabu ya AFC Leopards kuboresha kikosi chao yamepata pigo kubwa baada mchezaji wao wa zamani kuliandikia barua shirikisho la soka ulimwenguni FIFA na kuizuia klabu hiyo kusajili mchezaji yeyote.

• Beki wa timu ya taifa Harambee Cliff Nyakeya (Wazito), na kinda Victor Omune (KCB) pia walikuwa katika mipango ya kusajiliwa.

Mashemeji Derby
Image: Hisani

Matumaini ya klabu ya AFC Leopards kuboresha kikosi chao yamepata pigo kubwa baada mchezaji wao wa zamani kuliandikia barua shirikisho la soka ulimwenguni FIFA na kuizuia klabu hiyo kusajili mchezaji yeyote.

Mabingwa hao mara kumi na tatu wa ligi kuu nchini Kenya walikuwa na azma ya kushinda taji la ligi hiyo iwapo wachezaji wapya wangetua kambini humo.

Katika mahojiano Jumatatu, kocha msaidizi wa klabu hiyo, Tom Juma alisema kwamba walikuwa wameamua kuwasajili Josephat Lopaga kutoka Posta Rangers na straika matata kutoka klabu ya Polisi, John Makwatta.

Beki wa timu ya taifa Harambee Cliff Nyakeya (Wazito), na kinda Victor Omune (KCB) pia walikuwa katika mipango ya kusajiliwa.

Juma aliweka wazi kwamba wachezaji hao wanne walikuwa wameonekana kukubali kujiunga na na AFC na hata kufanya mazoezi nao.

“Juhudi za kuwaleta Lopaga, Makwata na Nyakeya kwenye klabu yetu yalilenga kuboresha safu yetu yan ushambulizi ambayo imetupelekea kupoteza na kutoka sare katika michuano yetu,” alisema Juma.

Hata hivyo Juma ameonyeshwa kusikitishwa kwa kile anachokitaja kama juhudi zao  kuponzwa na barua iliyoandikwa kwa FIFA na aliyekuwa mchezaji wao kutoka taifa la Rwanda, Soter Kayumba akitaka klabu hiyo kumlipa kima cha shilingi milioni 1.8, pesa ambazo anaidai klabu ya AFC.

Barua ya Kayumba iliwasukuma FIFA kuwapiga marufuku AFC kufanya usajili mwezi Machi mwaka jana , licha ya kubainika kuwa kulikuwa na wachezaji wengine zaidi waliokuwa wanaidai AFC.

Baadhi ya wale wanaoidai klabu hiyo ni pamoja na: Erstwhile gaffers Marko Vasiljevic, Andre Cassa Mbungo (Yupo Bandari kwa sasa), na wachezaji wa zamani katika kambi ya mwanachui, Kayumba, Vincent Habamahoro, naTressor Ndikumana.

Hata hivyo Juma ameweka wazi kwamba kuna mikakati kabambe ya kuhakikisha kwamba wanalipa madeni hayo ili kujiondoa katika minyororo hiyo ya FIFA.

“Tunasaka hela kukamilisha madeni hayo iwapo rufaa yetu itakubalika,” Juma alisema.

Licha ya mihangaiko na changamoto hizo, mwanachui alisajili ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Posta Rangers ugani Thika.

The win fired Leopards to 11th on the log, momentarily salvaging them from a relegation threat that had hounded them for the better part of the season.

“Tuna furaha kutokana na hatua klabu inazozipiga, na tunaamini tutasajili matokeo tuliyopata dhidi ya Rangers katika michuano yetu inayofuata,” Juma aliongezea.

Vilvile Juma amesema kwamba watajituma zaidi kuhakikisha kwamba wanajiondoa katika tanuri la kushushwa daraja msimu huu na kwamba wanaweza tu kufanya hivyo iwapo watafanikiwa kuboresha kikosi cho cha sasa.

Kulingana na Juma, kiungo mshambulizi, Collins Sichenje atakuwa anajiunga na kikosi hicho baada ya kutafuta unga na PAOK FC ya Ugiriki kwa miezi sita.

 

 

View Comments