09 August 2022 1 Min Read
DP William Ruto wa kwanza kupiga kura Sugoi
Ruto alifika katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Koschei kabla ya saa 6:00 asubuhi
In Summary
• Ruto alifika katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Koschei kabla ya saa 6:00 asubuhi
Naibu Rais William Ruto amempigia kura Sugoi.
Mgombea urais wa Kenya Kwanza alifika katika kituo cha kupigia kura pamoja na mkewe Mama Rachel Ruto.
Maafisa wa IEBC walichukua bayometriki ya DP Ruto kabla ya kupiga kura katika kituo cha Sugoi.
Ruto alifika katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Koschei akiwa amevalia kawaida.
Wakenya leo wanapiga kura zao katika vituo tofauti vya kupigia kura.