In Summary

•Kwa uchaguzi uliofanyika mnamo Agosti 9, Nicholas Gumbo alishindana na James Orengo kwa lengo ya kuwa gavana wa Siaya.

KiongozI wa ANC, mwanasiasa Gumbo na viongozi wengine
Image: Handout

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amekutana na aliyekuwa mbunge wa zamani wa Rarieda Nicholas Gumbo.

Gumbo ambaye aliwania kiti cha gavana wa kaunti ya Siaya kwa tiketi ya chama cha UDM na kupoteza kwa Seneta James Orengo alikuwa ameandamana na gombea mwenza David Ohito kwa mkutano kwenye makao makuu ya chama cha ANC.

Duru zaarifu kuwa mkutano huo ulijadili mikakati ya mwanasiasa huyo kuungana na Muungano wa Kenya Kwanza. Chama chake cha UDM tayari kimetia saini mkataba wa ushirikiano na muungano wa Kenya Kwanza baada ya kutangaza kugura Azimio.

Alipokelewa na Kiongozi huyo wa ANC ambaye pia ni mmoja wa vinara wa Kenya Kwanza.

Gumbo aliwania kiti hicho cha ugavana wa Kaunti ya Siaya na kushindwa na seneta James Orengo wa ODM.

Mwanasiasa huyo alikuwa kiwania wadhifa huo kwa mara ya pili baada ya kukosa kufua dafu mwaka 2017.

Katika jaribio la kwanza alishindwa na Coronel Rasanga ambaye alikuwa akiwania kiti hicho kwa muhula wa pili.

 

View Comments