In Summary

•Manoti alisema walikosana na baba yake mwezi uliopita wakati alimkataza kuuza shamba ya familia ili kujengea mke wake wa pili.

•Alisema kwamba tangu babake atoke nyumbani hajapata amani na angependa waweze kurejesha uhusiano mzuri.

•Mzee Philip alifichua mkewe wa kwanza ambaye ni mamake Manoti aliondoka takriban miaka kumi iliyopita na kumuachia watoto na hapo ndipo alifanya maamuzi ya kuoa mke wa pili.

Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho jamaa aliyejitambulisha kama Amos Manoti (22) kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba yake Philip Nyakundi (46)  ambaye walikosana mwezi mmoja uliopita baada ya  kuvurugana.

Manoti alisema walikosana na baba yake mwezi uliopita wakati alimkataza kuuza shamba ya familia ili kujengea mke wake wa pili.

Alisema babake hakuridhishwa na kitendo chake cha kumzuia kuuza shamba na hapo wakaanza kuvurugana kisha baadae mzee yule akafanya maamuzi ya kutoroka nyumbani kuelekea upande wa Migori pamoja na mke wake wa pili.

"Baba alitaka kuoa mke wa pili kwa sababu mama hayuko nyumbani. Walikosana kidogo na mama akaondoka kwa sasa hayuko nyumbani. Mzee alitaka kuuza shamba nikafikiwa na ripoti nikaenda kuharibu mipango. 

Nilienda nikamkataza baba nikamwambia hiyo haiwezekani. Baba alianza kunigombanisha. Aliniuliza mbona nilienda pale na sikuambia yeyote eti naenda. Tulianza kutupiana maneno. Walitoroka nyumbani wakaenda Migori na huyo bibi mwingine. Shamba alipewa na babu" Alisema Manoti.

Manoti alikiri kwamba walipokuwa wanakorofishana alitumia kiboko kumpatia babake kichapo ili kujilinda na kulipiza kisasi. Alisema kwamba tangu babake atoke nyumbani hajapata amani na angependa waweze kurejesha uhusiano mzuri.

Bwana Philip alipopigiwa simu Manoti alijitetea na kumuomba msamaha huku akidai alikuwa amejuta matendo yake sana.

Mzee Philip alifichua mkewe wa kwanza ambaye ni mamake Manoti aliondoka takriban miaka kumi iliyopita na kumuachia watoto na hapo ndipo alifanya maamuzi ya kuoa mke wa pili.

"Niliona siwezi kukaa hivo nikaleta mke mwingine. Kuleta mwingine sijui Manoti aliambiwa na nani ati nilitaka kuuza shamba . Alifika akaniweka ngumi, akaniweka chini na kunipiga na panga. Vile aliniumiza nilienda hospitalini nikatibiwa . Niliona siwezi kukaa nao nikaona ni heri niende kuishi kwingine na amani" Mzee Philip alisema.

Alimwagiza mwanawe aombe Mungu msamaha kisha baada ya hayo atafute siku washiriki kikao wasuluhishe mzozo wao.

Manoti alisema alikuwa amejuta yote ambayo alifanya huku akiahidi babake kuwa hangerudia kosa kama lile iwapo angekubali kumssamehe.

View Comments