In Summary

• "Mke wake alianza kumshuku baada ya kupunguza kiasi cha pesa ambacho alikuwa anaacha nyumbani." - Khaemba.

• Mke wake alisema hawezi kurudi huku akimpa Khaemba ruhusa ya kutafuta mke mwingine.

Ghost Mulee studioni
Image: RADIO JAMBO

Emmaul Khaemba mwenye umri wa miaka 47 alitaka kupatanishwa na mke wake wa miaka 33 ambaye walikuwa wamekaa kwa ndoa kwa miaka 10.

Khaemba alieleza kwamba mke wake aliamua kuondoka zake na watoto wote wane baada ya kumshuku kuwa alikuwa na mchepuko.

"Mke wake alianza kumshuku baada ya kupunguza kiasi cha pesa ambacho alikuwa anaacha nyumbani."

Kwa mara ya kwanza, Khaemba alimwambia mtangazaji Ghost kwamba kiasi cha pesa kilipungua kutokana na ugumu wa maisha lakini baada ya Ghost kumuuliza kwa undani, Khaemba alikubali kuwa alikuwa na mchepuko ambaye alikuwa anagawanya mapato yake baina ya familia yake na mchepuko.

“Alikuwa ananishuku eti pesa nilikuwa napeleka mahali kumbe si hivyo ni hali ngumu ya maisha tu pesa kupungua… pesa sikuwa napeleka mahali….Nilikuwa nimeshika mtu mahali, lakini sasa vile nafikiria nataka nilee watoto na yeye sitaki mambo mengine ….huyo mchepuko ako lakini nimekaa nimeona sikuwa nafanya vizuri, nataka nikae na familia yangu kwa sababu naona naendelea kuzeeka na huku mbele nisiporudi na familia yangu sitapata mtu wa kunisaidia,” Khaemba alisema.

 Kwa upande wake, mke wake Nafula alikataa kuwa si yeye baada ya kupigiwa simu, akisema hamjui mtu anaitwa Khaemba lakini baada ya bembeleza, Nafula alisema hakuwa anataka kusikia kitu chochote kutoka kwa Khaemba.

“Sitaki kusikia mambo yako kabisa wewe si mume wangu, unajua niko kazi wewe?” Nafula alisema kwa hasira za mkizi.

Alisema kwamba Khaemba alikuwa anatoa shilingi 300 pekee kwa ajili ya matunzo na karo ya watoto wote, watatu wakiwa shule za kibinafsi na mdogo akiwa nyumbani.

Pia alisema mume wake alikuwa anacheza na watoto wadogo kwenye mtaa walikuwa wanaishi mpaka akawa haheshimiki kabisa.

“Alikuwa anatoka kimapenzi na watoto wadogo na kina mama wazee katika mtaa tulikokuwa tunaishi mpaka sikuwa naheshimika na watu. Sina haja na msamaha wake, hata watoto wake akitaka awasaidie au asiwasaidie ni sawa mimi sitaki kusikia kitu chochote na yeye,” Nafula alisema.

Alimruhusu Khaemba kuoa mke mwingine kama anataka, akisema kwamba hataki kabisa kurudi kwake.

View Comments