In Summary

•"Msichana alianza kuhanyahanya nje. Tukakosana. Nilidhani ameenda nyumbani. Kumbe alienda kazini," Godfrey alisimulia.

•Mkewe Godfrey, Bi Ivy Chepkorir alifichua kwamba mama yao aliwaambia wasiwahi kumpigia simu.

GIDI NA GHOST
Image: RADIO JAMBO

Godfrey Achami mwenye umri wa miaka 28 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwe wake.

Godfrey alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika baada ya kurudiana na mke wake.

"Tulipata mtoto wa kwanza, mtoto akakufa, mke akanikosea. Wakati msichana alikuja akanikosea, nilifukuza yeye. Msichana alianza kuhanyahanya nje. Tukakosana. Nilidhani ameenda nyumbani. Kumbe alienda kazini," Godfrey alisimulia.

"Mama yake akanitafuta akisema anataka msichana wake. Mimi nikamwambia nilimfukuza. Baadaye nilitafuta msichana tukarudiana baada ya mwaka mmoja. Mama alisema hataki maneno yetu, tuongee na baba. Baba huwa tunaongea," aliongeza.

Mkewe Godfrey, Bi Ivy Chepkorir alifichua kwamba mama yao aliwaambia wasiwahi kumpigia simu.

Aidha, alikiri kwamba uhusiano wake na mamake uliharibika baada ya kukataa kwenda chuo.

"Aliniambia nisiwahi kumpigia simu. Tulikosana na mama. Alikuwa amenitafutia nafasi shule polytechic nikatoroka. Kuna kazi alikuwa amenitafutia nifanye kidogo ndio tupate karo, nikatoroka. Nataka kukaa kwa ndoa," Ivy alisema.

Juhudi ya kuwapatanisha wapenzi hao na mama yao hata hivyo hazikufua dafu kwani alikuwa amezima simu.

Godfrey alisema, "Mama mkwe mimi sina ubaya na sijawahi kukosea. Mimi nakuomba tuongee, tukubaliane kama wazazi wangu watakuja nyumbani tuongee."

Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?

View Comments