In Summary

•Jared alibainisha kwamba tangu kuzaliwa kwake hajawahi kuwa na uhusiano wa karibu na babake kwani alitengana na mamake akiwa mdogo sana.

•"Nilikuwa nataka angalau anipeleke kwake. Saa hii nikifa nitapelekwa wapi? Mama yangu hatuwezi kupatana. Ananijua tu vizuri,' alisema.

Gidi na Ghost Studioni
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Alex Juma ,28, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba yake Jared Maseli mwenye umri wa miaka 56.

Jared alibainisha kwamba tangu kuzaliwa kwake hajawahi kuwa na uhusiano wa karibu na babake kwani alitengana na mamake akiwa mdogo sana.

"Babangu hatujawahi ishi naye pamoja. Mamangu alinionyesha yeye lakini hajawahi kunikubali vizuri. Nikimpigia simu hashiki. Nilijaribu kuomba mjomba wangu atupatanishe lakini baba hajawahi kunikubali kama mtoto wake. Mama aliolewa na mwanaume mwingine," Jared alisimulia.

Aliongeza, "Mama alinitambulisha kwa baba nikiwa na umri wa miaka 20. Tulienda mazishi ya mama ya baba, tulikaa na baba vizuri wakati huo ata nilidhani anataka kuenda na mimi. Sasa hivi, simu zangu hashikangi."

Jared alilalamika kwamba hana mahali pa kuita nyumbani, jambo ambalo linamtia wasiwasi.

"Mimi nilikuwa nataka angalau baba yangu ananitambua. Nilikuwa nataka angalau anipeleke kwake. Saa hii nikifa nitapelekwa wapi? Mama yangu hatuwezi kupatana. Ananijua tu vizuri,' alisema.

Juhudi za kumpatanisha Jared na baba yake hata hivyo hazikufua dafu kwani mzazi huyo wake hakupatikana kwa simu.

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?

View Comments