logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize amtupia Diamond vijembe huku akiimba wimbo wake wa 'Wapo'

“…Baba na Mama ndio nguzo ya Dunia, watunze!! Sio Baba Dangote Analia

image
na Radio Jambo

Yanayojiri14 January 2021 - 21:32

Muhtasari


  • Harmonize amtupia Diamond vijembe huku akiimba wimbo wake wa 'Wapo'
  • Harmonize amkejeli Diamond kwa kutomsaidia baba yake
hamo 1

Msanii Harmonize yuko bizi huku akimtupia aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz vijembe.

Msanii huyo alifanya hayo alipokuwa akiwaburudisha wananchi wa Zanzibar akiimba kinao chake cha 'wapo' alimkashifu Simba kwa kumtenga baba yake.

“…Baba na Mama ndio nguzo ya Dunia, watunze!! Sio Baba Dangote Analia, naye Mama Dangote Anacheka Cheka, oooh, kuna watu na vitu duniani." Aliimba Harmonize

 

Baada ya kutoa kibao chake mwaka jana mashabiki wengi walimshambulia huku wakisema kwamba amemkosea Diamond heshima.

Hii hapa mistari ya kibao chake cha Wapo.

"Kama Baba na Mama ndio Nduzo ya Dunia, wapende wote, sio eti wa Kike anacheka, na wakiume analialia hana msaada wowote, ooh oooh, kuna watu na vitu wanatamani milele wawe wao, ukijituma watasema unashindana nao

Ooh, ni kama watu, kumbe ndani wana roho za chatu, hawatosheki na vikubwa vyao, wanatamani hata kidogo chako kiwe chao."

Si mara ya kwanza Harmonize kutoa kibao huku akimkejeli Diamond.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimkejeli Harmonize na kusema kwamba hajielewi baada ya kutoka katika lebo ya WCB.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved