Buriani:Orodha ya wanasiasa walioaga dunia mwezi wa februari 2021

Muhtasari
  • Wanasiasa ambao wameaga dunia mwezi ya Februari 2021
  • Mwaka wa 2021 tumeshuhudia na kusikia vifo vya watu mashuhuri haswa katika sekta ya siasa
Seneta Yusuf Haji

Kifo ni jambo ambalo mtu yeyote hawezi tamani litokee katika familia au kwa mtu yeyote, lakini msanii mmoja hakukosea aliposema kwamba kaburi nitajiri.

Mwaka wa 2021 tumeshuhudia na kusikia vifo vya watu mashuhuri haswa katika sekta ya siasa.

Kuna baadhi ya wanasiasa ambao wameaga dunia mwezi wa februari huku nchi nzima ikiomboleza vifo vyao;

 

Hii hapa orodha ya wanasiasa ambao wameaga dunia mwezi wa Februari mwaka 2021, ni mwei ambao unafahamika wa mapenzi kwa ajili ya siku ya wapendanao lakini kwa wengi ulikuwa mwei wa huzuni.

Pia unapendwa na wengi kwa maana ni mwezi mfupi katika miezi ya kalenda;

1.Simeon Nyachae

Nyachae alizaliwa manamo mwaka wa 1932, katika kaunti ya Kisii, alikuwa mwanasiasa nyakati za mwendazake Daniel Arap Moi.

Simeon-Nyachae
Simeon-Nyachae

Mwanasiasa huyo aliaga dunia mnamo tarehe 1 Februari mwaka wa 2021.

2.Francis Waititu

Alikuwa mbunge wa Juja ambaye kifo chake ni cha awali, Waititu aliafa dunia tarehe 22 Februari 2021 baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

 

3.John Oroo Oyioko

Oroo aliaga saa chache baada ya aliyekuwa waziri Simeon kuzikwa nyumbani kwake,Familia yake ilisema kwamba aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Ada Khan kaunti ya Kisumu.

Marehemu mbunge wa Bonchari John Oroo Oyioka
Marehemu mbunge wa Bonchari John Oroo Oyioka

Alikuwa mbunge wa Bonchari, aliaga dunia tarehe 15 Februari 2021.

4.Yusuf Haji

Alikuwa seneta wa kaunti ya Garissa tangu mwaka wa 2013, bali na kuwa seneta alikuwa mwenyekiti wa mipango ya maridhiani BBI, alizaliwa mwaka wa 1940.

Seneta Yusuf Haji

Yusuf aliaga dunia Februari 15 2021,akiwa katika hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipokea matibabu.

4.Hosea Kiplagat

Alikuwa mwanasiasa enzi za mzee Moi, aliaga dunia februari 6, alipokimbizwa katika hospitali ya Karen

Mungu azidi kulaza roho zao mahali pema peponi.