Kuwa katika tasnia ya burudani haswa wanawake ni ngumu sana,na wengi wao hupitia changamoto tofauti.
Bali na changamoto ambazo wanawake hao hupitia wametia bidii katika kazi yao ya burudani, kila pande katika muziki,ucheshi na sekta zingine za burudani.
Hii hapa orodha ya wanawake ambao wametikisa tasnia ya burudani nchini kenya, na wanazidi kutia bidii, kuwafurahisha mashabiki wao;
1.Nadia Mukami
Nadia ni mwanamke ambaye anaendelea kutia bidii, katika kazi yake ya usanii huku akipeperusha bendera katika kazi hiyo.
Msanii huyo amefanya colabo na wasanii tofauti huku nymbo zake zikipenwa sana na wakenya hata nchi za nje.
2.Cartoon
Mchekeshaji huyo wa kipindi cha churchill, licha ya nchi na maeneo ya burudani kufungwa amekuwa katika mstari wa mbele kuwafurahisha na kuwachekesha mashabiki wake na wakenya kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya youtube.
3.Vivian
Mwanamuziki huyo amekuwa akitoa kibao kimpja baada ya kingine,ni mwanamke mwenye urembo wa kipekee.
4.Tanasha Donna
Ni mwanamke ambaye ameonyesha bidii katika tasnia ya muziki, huku akitoa colabo na wasanii tofauti nchini na hata nje za nchi.
5.Femi One
Ni mwanamuziki wa kipekee ambaye amevuma sana kwenye tasnia ya burudani, na mwenye bidii yake.