'Akon ananitambua sasa,'Akothee asema baada ya kuwa miongoni mwa wasanii tajiri Afrika

Muhtasari
  • Orodha ya wasanii tajiri Afrika imetolewa na imekuwa ikisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii
  • Miongoni mwa wasanii walioorodheshwa ni Wizkid,Davido,Burnaboy, huku msanii Akothee akiwa nambari 15
  • Akothee ajisifia baada ya kutajwa miongoni mwa wasanii tajiri Afrika
akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)

Orodha ya wasanii tajiri Afrika imetolewa na imekuwa ikisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa wasanii walioorodheshwa ni Wizkid,Davido,Burnaboy, huku msanii Akothee akiwa nambari 15.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee alifurahia matokeo hayo huku akisema kwamba msanii Akon kutoka Marekani amemtambua sasa.

"KENYA MTAJITETEA MKIWA UPANDE GANI. 40 looks like this 🤣🤣

Msanii tajiri Afrika,hawajasema mwanamke  , wamesema msanii tajiri omesikia hiyo i ?Wakenya hawatakubali 🤣🤣🤣🤣 watasema pia  bilgatesni tajiri na hasemi ! wewe ulijuaje ?Watasema nimelipa Forbes.🤣🤣lakini sio kenya waliniuza kitambo sanawalinibadilisha na wasanii wengine ambao huwa wanawatamani.

Walinipeana na watoto wangu pamoja na mbwa wangu🤣🤣🤣🤣🤣SHIDA ni AKOTHEE tuu ndio ako availableWatado 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣,"Akothee Aliandika.

Mwanabiashara huyo alipakia picha ya orodha hiyo, huku akisema kuwa msanii Akon anamtambua sasa.

Hii hapa orodha ya hiyo;