logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Nitakuja kwako usipokuja kwangu,'Msanii Nyota Ndogo azidi kumbembeleza mumewe

Nyota waliachana na mumewe mwezi wa Aprili, baada ya siku ya 'Fools day'.

image
na Radio Jambo

Habari15 May 2021 - 07:32

Muhtasari


  • Msanii Nyota Ndogo amezidi kumbembelea mumewe kwa kumwandikia ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram na kumsihi akumbuke umbali wametoka
  • Pia msanii huyo aliweka wazi kuwa atapigania mapenzi yao, kwa maana hawezi ishi bila mumewe
  • Nyota waliachana na mumewe mwezi wa Aprili, baada ya siku ya 'Fools day'
nyota ndogo

Msanii Nyota Ndogo amezidi kumbembelea mumewe kwa kumwandikia ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram na kumsihi akumbuke umbali wametoka.

Pia msanii huyo aliweka wazi kuwa atapigania mapenzi yao, kwa maana hawezi ishi bila mumewe.

Nyota waliachana na mumewe mwezi wa Aprili, baada ya siku ya 'Fools day'.

"Nitajaribu kuandika kingereza ndio ashikanishe. Hata kama kizungu yangu sio nzuri I will fight for this love

Watu wanafikiria nirahisi penzi ulilolizoea unaweza kuliacha gafla nop not me. Mimi nalia mtandaoni kuna wanaojinyonga kwakuogopa kuongea wacha waseme najiaibisha lakini KAMA KUKUPENDA NIMAKOSA SITAKI KUA SAWA DUNIANI," Aliandika.

Baada ya Nyota kufunga pingu za maisha na mumewe, alfichua kwamba walipoka kejeli nyingi huku baadhi ya mashabiki wakidai kwamba anakaa mfu ambaye amefufuka.

Licha ya hayo yote mumewe alimtia nguvu huku akimwambia kwamba yeye ni mrembo.

Mpenzi wangu unakumbuka siku hii? hii ilikuwa siku ambayo mwili wetu ulikuwa mmoja  lakini pia this day Pia ilikuwa siku ambayo tulikejeliwa yani tulipuliwa mpaka tunaenda mlima wa sagala kusoma maoni

Nilikuwa na soma yale watu walikua wanacooment lakini  unakumbuka jumbe moja ulisoma ilikua inasema NYOTA UNAKAA KAMA MFU AMEFUFUK

nikakusomea nikatranlate what you after me reading for you you hold me tight yani very tight then you said to me YOUR BEAUTIFUL my wife

UMENIBLOCK KILA MAHALI LAKINI GOOGLE itakupa ujumbe I will come to you if you don’t come here. Wewe mawe basi huna uruma Jamani,"

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved