DRAMA ZA APOKO

"Mimi pekee ndiye tajiri kuliko Diamond" Ringtone adai

Mwanamuziki Ringtone Apoko amemuunga mkono Diamond kuisuta Forbes kwa kutofanya utafiti dhabiti wa wasanii tajiri zaidi AfrIka

Muhtasari

•Ringtone adai kuwa yeye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi Afrika Mashariki

•Diamond aliisuta Forbes kwa kumtaja kama nambari ishirini na nane kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Image: Hisani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Alex Apoko almaarufu kama Ringtone amemuunga mkono Diamond kusuta shirika la Forbes.

Diamond aliisuta Forbes kwa kumtaja kama nambari ishirini na nane kwenye orodha ya wanamuziki tajiri mno Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ringtone amedai kuwa yeye pekee ndiye amempiku Diamond kwa utajiri eneo la Afrika Mashariki.

Ringtone pia ameiagiza shirika hilo la habari kuwahusisha wasanii wa nyimbo za injili.

Wakati mwingine Forbes shirikisheni wanamuziki wa injili wakati . Msiogope kuniweka kama nambari moja kwani huo ndio ukweli na ukweli utawaweka huru. Diamond ni nambari mbili Afrika iwapo wanamuziki wa injili watashilikishwa.” Ringtone aliandika kwa kiingereza kibovu.

Ringtone alikuja kutambulika zaidi mwakani 2009 baada ya kuwachilia wimbo ‘Pamela’. Ingawaje muziki wake haujakuwa ukivuma sana kw muda mrefu. Amekuwa akihusika kwenye drama si haba.

Rintone hata hivyo hakutajwa kwenye orodha ya wanamuziki thelathini tajiri zaidi Afrika.