Wasanii tajiri Afrika

Diamond aisuta Forbes

Diamond aliorodheshwa kama nambari 28 kwa utajiri na dhamana ya $5.1m, awaagiza Forbes kumchunguza vizuri wajue dhamana yake.

Muhtasari

•Forbes ilimtaja Diamond kuwa nambari ishirini na nane akiwa na dhamana ya dola milioni 5.1

•Youssu N'dour wa Ghana alitangazwa kama mwanamuziki yule tajiri zaidi Afrika

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: HISANI: Instagram

Msanii tajika wa  nyimbo aina ya Bongoflava, Diamond Platnumz ameisuta kampuni ya Forbes kwa kumuweka kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Mwanamuziki huyo tokea Tanzania amewasihi Forbes kufanya utafiti dhabiti kabla ya kuweka jina lake kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

 

Wakatimwingine mfanye utafiti mzuri ili mdhibitishe thamani yangu ya kweli kabla ya kuweka jina langu kwenye orodha yenu ya kishenzi ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika” Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kulingana na orodha iliyotolewa na shirika la Forbes hivi majuzi, Diamond hayupo miongoni mwa wanamuziki tajiri zaidi Afrika wa kwanza ishirini.