FAMILIA YA WAJESUS

Usizingatie sura ama pesa unapotafuta mchumba- Kabi

Kabi WaJesus ashauri watu kuoa marafiki zao wa dhati

Muhtasari

•Kabi wa Jesus akiri kuwa unapomuoa rafiki wadhati muda wote huwa 

•Milly amshukuru Yesu kwa kumpatia mume anayempatia mapenzi ya dhati

FAMILIA YA WAJESUS
FAMILIA YA WAJESUS
Image: HISANI; Instagram

Mburudishaji na vlogger  Peter Kabi almaarufu kama ‘Kabi Wa Jesus’ amewashauri vijana wasioe kwa ajili ya pesa au kuzingatia sura.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kabi ameshauri watu kuoa mtu ambaye anamfanya kufurahia. Amemtaja bibi yake Mily wa Jesus na ambaye  pia ni mchezaji mweza kwenye kipindi chao cha Youtube almaarufu kama  ‘Wajesus Family’ kuwa chanzo cha furaha yake.

“Unapomuoa rafiki wako wa dhati, kila  wakati huwa wakati wa raha” Kabi aliandika kwenye maelezo ya picha aliyoweka kwenye akaunti yake ya Instagram. Picha ile ilimuonyesha wakiwa na bibiye wakionekana watu waliojawa na furaha.

Kwa upande wake Milly, alimshukuru Yesu kwa kumpa mtu anayempa mapenzi tele.

“Ni bahati kubwa aje niliyopata? Asante Yesu kwa kunipa mume anayenishika mkono na kunipa mapenzi mengi” Milly alisema.

Wiki mbili zilizopita, Kabi alikiri kuwa alikuwa kapata mtoto na binamu yake. Jaribio la DNA lilibaini kuwa mburudishaji huyo ndiye baba halisi ya msichana wa miaka saba ambaye alikuwa amemkana hapo awali.