"Ningependa kujaribu kiumbe tofauti" Willy Paul asema

Mwanamuziki mashuhuri Wilson Radido almaarufu kama Willy Paul amewashangaza wengi baada ya kutangaza kuwa angependa kujaribu mapenzi na mgeni wa anga ‘aliens’

Muhtasari

•“Nimechoka, ningependa kushuhudia kitu tofauti, mkiona ‘alien’ mahali inatembea nijulisheni” Willy Paul aliambia mashabiki kupitia ukurasa wake wa Instagram

Willy Paul
Willy Paul

Mwanamuziki mashuhuri Wilson Radido almaarufu kama Willy Paul amewashangaza wengi baada ya kutangaza kuwa angependa kujaribu mapenzi na mgeni wa anga almaarufu kama ‘aliens’

Msanii huyo ambaye alipata umaarufu kwa kuimba nyimbo za injili kabla yake kurudi nyuma amewacha mashabiki vinywa wazi baada ya kudai kuwa ameshuhudia wanawake wa aina yote na kwa sasa angependa atafutiwe kiumbe wa anga.

Nimechoka, ningependa kushuhudia kitu tofauti, mkiona ‘alien’ mahali inatembea nijulisheni” Willy Paul aliambia mashabiki kupitia ukurasa wake wa Instagram. Soma baadhi ya hisia za Wakenya kwenye chapisho la Paul hapa chini

Mwanamuziki huyo ameendelea kuzungukwa na drama tele toka abadilishe mtindo wake wa usanii.