Wanawake wengi wapendezwa na Mcheshi Mjapani, Koki Nakaya

Mulamwah asema kuwa Koki ameteta kuwa wanawake Wakenya wamefurika kwenye DM yake

Muhtasari

•Koki amekuwa akishirikiana na Mulamwah kutumbuiza Wakenya

•Ameiga lugha na tabia nyingi za Wakenya

Mulamwah na Koki
Mulamwah na Koki
Image: Hisani

Mcheshi David Oyando almaarufu kama Kendrick Mulamwah ametangaza kuwa mcheshi mwenzake anayejitambulisha kama Koki Nakaya amekuwa akipokea jumbe nyingi toka kwa wanawake Wakenya.

Koki ambaye ni mzaliwa wan nchi ya Japani amekuwa akishirikishwa naye Mulamwah kwenye video zake za ucheshi na ameonekana kupendeza wengi.

Anateta kuwa mmejaa kwenye DM yake” Mulamwah alimjibu shabiki mmoja aliyeomba kupatanishwa na Mjapani yule.

Mulamwah na Koki
Mulamwah na Koki
Image: Hisani

Hizi hapa baadhi ya video za wawili hao

Wakenya wengi wamependezwa na ucheshi wake Koki huku akionekana kuiga lugha na tabia nyingi za Wakenya.