ULAGHAI MTANDAONI

"Laghaiwa kwa gharama ya akili yako ndogo" Zari awaambia wanaokubali kulaghaiwa

Mwanasosholaiti Zari Hassan awaonya wanaolaghaiwa na mikora inayotumia jina lake

Muhtasari

•Zari amesema kuwa yeye huwa haombi msaada wa fedha wala kupeleka watu ughaibuni

•Asema huwa hatumi jumbe za Facebook na Instagram wala kujibu jumbe anazotumiwa

Zari Hassan
Zari Hassan
Image: HISANI

Mwanasosholaiti na mwanabiashara maarufu Zari Hassan amewaonya watu wanaolaghaiwa mitandaoni na wakora wanaojitambulisha kama yeye.

Zari ambaye alikuwa mpenzi wake Diamond Platnumz amesema kuwa hatokubali kamwe kukubali wajibu kwa tendo asilohusika.

“Huwa siombi msaada wowote wa kifedha na siwapeleki watu ughaibuni. Siagizi pesa zozote kufanya  Zari, sifanyi hilo” Zari aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Binti huyo mzaliwa wa Uganda ameonekana kukasirishwa na kitendo cha mmoja wa wakora wanaomuiga kulaghai watu na kisha waliolaghaiwa kumtumia Zari barua pepe wakidai kurudishiwa fedha zao.

Wanaonijua wanaelewa kuwa huwa situmi jumbe za Facebook na huwa sijibu jumbe ninazopokea kwenye mtandao huo.” Zari alisema huku akimueleza aliyelaghaiwa aonyeshe nambari ya WhatsApp aliyokuwa anazungumza nayo.