HERI ZA KUZALIWA BI MUSILA

Guardian Angel asifia mpenziwe akiadhimisha kufikisha miaka 51

“Nilikuwa pweke ukajaza nafasi hiyo. Nilikuwa sijakamilika ukaja ukanikamilisha. Nilikuwa karibu kukosa matumaini na uimbaji wangu ukaja wakati ufaao na kwa kipindi kifupi ukabadilisha kila kitu na maisha yangu ikarudi laini”- Guardian Angel

Muhtasari

• Guardian Angel, 30,amesema kuwa Bi. Musila alikuja wakati alikuwa karibu kupoteza matumaini akamsaidia kuinuka.

• Musila pia amewashukuru wanawe watatu kwa kumuonyesha mapenzi tele na kumshikilia.

Guardian Angel na Esther Musila
Guardian Angel na Esther Musila
Image: Instagram

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Peter Omwaka almaarufu kama Guardian Angel ameandika ujumbe kumsifia mpenzi wake Esther Musila katika siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake huku akiadhimisha kufikisha miaka 51.

Katika ujumbe huo ambao alichapisha kwenye ukurasa wa Instagram, Guardian Angel, 30, amemwarifu Bi Musila kuwa hajakuwa na shaka yoyote kuwa yeye ndiye kipenzi chake tangu  kupatana kwao.

“Nilikuwa pweke ukajaza nafasi hiyo. Nilikuwa sijakamilika ukaja ukanikamilisha. Nilikuwa karibu kukosa matumaini na uimbaji wangu ukaja  kwa wakati ufaao na kwa kipindi kifupi ukabadilisha kila kitu na maisha yangu ikarudi laini” Guardian Angel alimwandikia Musila.

Wawili hao ambao ni wanamuziki wamekuwa kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

“Umenifanya kuamini kuwa kuna mapenzi ya kikweli. Inashangaza jinsi unavyonipenda. Naweza endelea mpenzi wangu ila kwa sasa wacha nikutakie baraka” Alimwandikia Angel huku akimtakia heri za kuzaliwa.

Kwa upande wake Musila, amemshukuru Mungu kwa kumletea mpenzi wake na kusema kapendezwana safarii ile. Pia amewashukuru wanawe watatu kwa mapenzi na kumshikilia. Amesema kuwa yeye si 51 ila yeye ni 21 na miaka 30 ya uzoefu.