EMBARAMBAMBA ATOKEA KUJIELEZA

"Nilikuwa naigiza ujumbe wa wimbo!" Embarambamba hatimaye ajitetea

Embarambamba amewakashifu wanamhukumu kutokana na video zinazozunguka huku akieleza kuwa alikuwa anaigiza tu vitendo za ujinga ziinazotajwa kwenye wimbo

Muhtasari

•Amewaagiza Wakenya kuelewa ujumbe wa wimbo kabla ya kumhukumu.

•Amepeana mfano kutoka kwa Biblia akieleza kuwa Yesu pia alikaa na washerati ili awaokoe

Chris Embarambamba akitoa ujumbe wake
Chris Embarambamba akitoa ujumbe wake
Image: Hisani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Chris Embarambamba amejitokeza kujieleza kuhusiana na video zinazosambazwa mitandaoni na Wakenya.

Kupitia kwa ujumbe ambao ametoa kupitia mtandao wa Youtube, mwanamuziki huyo amewakashifu wanamhukumu kutokana na video hizo huku akisema kuwa alikuwa anaigiza tu ujumbe uliokuwa kwenye wimbo.

Embarambamba ameeleza kuwa wimbo huo unazungumzia maovu ambayo yanafanyika duniani. Amewaagiza Wakenya kuelewa ujumbe wa wimbo kabla ya kumhukumu.

“Wakenya wamenihukumu, Wakenya wamenitusi, mashabiki wangu wamekasirika, wengine wanasema mimi ni Shetani eti sijaokoka ila ningataka Wakenya waskize ujumbe ulio kwa wimbo huo nilikuwa naimba. Wimbo unasema umetoa wapi huu ujinga wa kufanya vitendo kama hivi wapi, umesahau Mungu kwa msalaba?” Embarambamba alisema huku akieleza kuwa alikuwa anaigiza ujinga ambao anazungumzia kwa wimbo.

Kwenye video hizo, Embarambamba alionekana akiwa kwenye klabu akicheza densi zisizo na nidhamu na mashabiki wake. Video moja ilimuonyesha msanii huyo kutoka Nyamira akiwa amemlaza mwanadada chini na kuchezea densi juu yake.

Video nyingine ilimuonyesha Embarambamba akiwa ameinua mwanaume mmoja juu nakumuweka kwenye kiuno chake na kucheza densi isiyoridhisha macho.

Mwanamuziki huyo ameeleza kuwa alikuwa amehudhuria sherehe iliyokuwa karibu na Thika Road.

Amepeana mfano kutoka kwa Biblia akieleza kuwa Yesu pia alikaa na washerati ili awaokoe.

“Huwezi sema ati Embarambama usiende kwenye klabu au mikutano ya siasa kwani sote tuko kwa hii dunia na Yesu alituweka huku tumfuate na Kumtii” alisema Embarambamba.

Wanamitandao wameendelea kumkashifu huku wakimtaka aombe msamaha badala ya kujaribu kuhalilisha matendoyake.