Mcheshi na mtangazaji wa radio, Herman Kago almaarufu kama Profesa Hamo ametangaza hadharani kuwa ana mipango ya kumuoa Jemutai.
Alipokuwa anashirikisha mashabiki kwenye kipindi cha maswali na majibu(Q&A) kwenye mtandao wa Instagram, Hamo alithibitisha kuwa angemuoa mchechi mwenzake, Stella Bunei ajulikanaye kwa jina la jukwaa kama Jemutai kuwa mke wa pili kwani wametoka mbali.
Shabiki: Je, utamuoa Jemutai kama mke wa pili? naamini kuwa ni mwanamke mrembo na mwenye bidii.
Hamo: Ndio.. tumetoka mbali sana.
Hamo alimjibu shabiki mwingine aliyetaka kujua kama wamesuluhisha mgogoro uliokuwa baina yake na mama watoto(Jemutai) kuwa yeye sio mama watoto ila ni mke wake.
Shabiki:Je, mmesuluhisha ugomvi baina yako na baby mama wako?
Hamo: Yeye sio baby mama wangu, ni mke wangu!
Awali wiki iliyopita, mcheshi huyo tajika alitumia mitandao ya kijamii kuomba msamaha hadharani kutokana na matendo yake ya kutelekeza wanawe wawili ambao wamepata na Jemutai.
Maneno yote yalitokea hadharani baada ya Jemutai kukiri mtandaoni kuwa ana watoto wawili na mcheshi Hamo aliyekuwa mtangazaji mwenza wa Jeff Koinange katika kipindi cha asubuhi kwenye stesheni ya radio ya Hot 96.
Kwa kwanza Hamo alikuwa amekanusha madai ya kutelekeza wanawe ila akaonekana mwenye kujirudia baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kuwa yeye ndiye baba halisi ya watoto wale.
Hamo alipongezwa sana na mashabiki kuhusu namna alisuluhisha ugomvi baina yao.
Shabiki: Nina furaha sana kuwa mlisuluhisha maneno yenu. Nyinyi wawili mtakuwa wanandoa wazuri.
Shabiki:Je, mapenzi yaweza yakarejea baaada ya mgogoro kutangazwa hadharani.
Hamo: Ni wawili wapendanao ambao hugombana.
Kwa upande wake Jemutai alikiri kuwa amemsamehe Hamo baada ya kipindi cha usuluhisho na kuelewana kati yao.
Shabiki: Je, ulimsamehe Hamo
Jemutai: Naam.
Wanamitandao wengi wameendelea kuwapongeza wawili hao na kuwatakia mazuri maishani.