MASAIBU YA EMBARAMBAMBA

"Nyanyake alikuwa mchawi!" Ringtone amkashifu Embarambamba

Ringtone amedai kuwa sarakasi nyingi anazocheza Embarambamba kwenye nyimbo zake zilitokana na tabia za kiuchawi alizofunzwa na marehemu nyanyake

Muhtasari

"Embarambamba alibeba tabia ambazo alifunzwa na nyanyake kuhusiana na vile uchawi hufanywa kama vile kuning'inia kwa miti na kupanda paa za nyumba akafikiria ni talanta na kuzileta kwa nyimbo za Mungu" Ringtone alisema.

•Amewaagiza Wakenya kusita kuharibia wasanii wa injili jina huku akisema kuna baadhi yao wanaotia bidii sana kazini kuhakikisha kuwa injili inaheshimika.

Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Image: Hisani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Ringtone Apoko almaarufu kama Ringtone ametokea kukashifu Embarambamba kutokana na video zinazozunguka mitandaoni ambazo zinamuonyesha akishiriki kwenye densi zisizo za kimaadili na mashabiki kwenye klabu.

Ringtone ambaye anajitambulisha kama mwenyekiti wa wanamuziki wa nyimbo za injili nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa jumla amedai kuwa Embarambamba hajaokoka na kuwa sio mwanamuziki wa nyimbo za injili.

"Embaramba ni mwanabiashara, ametoka Kisii akiwa mcheza densi wa Sagero ambaye ni msanii mkubwa zaidi wa nyimbo za kidunia wa Wakisii" alidai Ringtone kupitia mtandao wa Instagram.

CHRIS EMBARAMBAMBA
CHRIS EMBARAMBAMBA
Image: HISANI: YOUTUBE

Apoko ameendelea kueleza kuwa mtindo wa densi wake Embarambamba unaohusisha sarakasi nyingi ulitokana na tabia za uchawi alizofunzwa na marehemu nyanyake.

"Embarambamba alitoroka Kisii akaja akaanza kufanya uwazimu, nimethibitisha kutoka kuwa nyanya yake alikuwa mchawi. Embarambamba alikuwa anampenda nyanyake sana kwa hivyo alipokufa alilia sana. Baadae, Embarambamba akabeba tabia ambazo alifunzwa na nyanyake kuhusu vile uchawi hufanywa kama vile kuning'inia kwa miti na kupanda paa za nyumba akafikiria ni talanta na kuzileta kwa nyimbo za Mungu" Ringtone alisema.

Ringtone ametangaza kuwa amethibisha kutoka Kisii kuwa Embarambamba aliathirika sana na kifo cha nyanyake aliyetaja kuwa mchawi kwani alimpenda sana.

Mwanamuziki huyo aliyekuja kutambulikana kutokana na nyimbo 'Pamela' na 'Tenda wema' amesema kuwa Embarambamba aliwachanganya mashabiki na sarakasi hizo za kiuchawi wakaamini kuwa ni talanta. Amewaagiza Wakenya kusita kuharibia wasanii wa injili jina huku akisema kuna baadhi yao wanaotia bidii sana kazini kuhakikisha kuwa injili inaheshimika.

"Tunataka kuhakikisha kuwa usanii wa nyimbo za injili umerudi juu ili wasanii wa nyimbo za kidunia wanaoharibu Kenya warudi mahali walitoka.. ili Khaligraph arudi alikotoka, Otile Brown arudi Mwembe Tayari Mombasa auze nguo, Nameless arudi kuwa msanifu majengo, Mejja arudi na wasanii wengine wote. Msituchanganye na wasanii wengine, Embarambamba si mmoja wetu" Ringtone alimalizia kwa kusema.