'Wachaneni na maisha ya watu,'Sonko awashambulia wanaomkejeli mkewe Guardian Angel

Muhtasari
  • Sonko awashambulia wanao mkejeli mkewe Guardian Angel

Msanii wa nyimbo za injili Guardian Angel alimvisha mpenzi wake pete ya uchuba JUmanne huku akisheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Esther Musila alipokea kejeli nyingi kwa sababu amemuacha msanii huo zaidi ya miaka 20.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amegadhabishwa na kejeli za wanamitandao, na kutetea uhusiano kati ya Guardian Angel na Esther Musila.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Sonko alisema kwamba watu wanapaswa kuachana na maisha ya wengine kama wanataka kuendelea.

"Mrembo huyu anaitwa Esther Musila anafanya kazi na UN ... ana miaka 51 .... jana alichumbiwa na mwanamuziki wa injili Guardian Angel wa miaka 30

Nimeona tu watu wenye nia mbaya wakimtia maneno mabaya kama bibi yake. Hii sio haki kabisa

Nyinyi mukitaka pia muowane ama muolewe wachaneni na maisha ya watu. Buree kabisa nyinyi

wewe Esher na Guardian Angel Hongera kwa ndoa yako, ninawatakia maisha ya Upendo na furaha. Miaka ijayo na ijazwe na furaha ya kudumu." Aliandika Sonko.

Licha ya kejeli nyingi kutoka kwa mashabiki wawili hao wamezidi kuonyesha kuwa 'Age is just a number' bali mapenzi ya kweli yanadumu.