RINGTONE ATISHIA GUARDIAN ANGEL

Ringtone aapa kumfichua Guardian Angel hadharani

Ringtone alisema kuwa Guardian Angel ni mnafiki na kuna mambo anayofanya ambayo atafichua siku ya Alhamisi.

Muhtasari

•Alisema  kuwa atahutubia wanahabari kuhusu vitu fiche ambazo  Guardian Angel anafanya

•Ringtone alimtaja Guardian Angel kuwa mnafiki

Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Image: Instagram

Mwanamuziki wa nyimbo za injili mwenye utata mwingi, Ringtone Apoko amemkashifu mwanamuziki mwenzake, Guardian Angel huku akimuita Mkristiano bandia.

Kupitia mtandao wa Instagram, Apoko ameapa kutoa ujumbe kwa wanahabari akimfichua Guardian Angel.

"Kesho naenda kumfichua Guardian Angel vibaya sana na nafikiria sasa ananenda kuisha. Kuna vitu amefanya na anajifanya bado, namfichua kesho" Ringtone alitangaza.

Mwanamuziki huyo ambaye anajitambulisha kama mwenyekiti wa wanamuziki wa nyimbo za injili amewaagiza Wakenya kusubiri uvumbuzi mkubwa kumhusu Guardian Angel.

"Kesho saa nne naita wanahabari, tayarisheni simu zenu, tafuteni wakati, ombeni ruhusa kutoka kazini kwani namfichua Guardian Angel na sina mchezo" Alidai Ringtone.

Msanii Guardian Angel alitoa ombi la ndoa kwa mpenzi wake, Esther Musila ambaye alisema NDIO. Tusubiri ujumbe wa Ringtone tuskie ana yepi ya kusema kumhusu Guardian Angel...