VANESSA NA ROTIMI

Vanessa Mdee na mwigizaji Rotimi waandika kitabu cha Kiswahili

Vanessa alisema kuwa amekuwa akitia bidii sana kumfunza Kiswahili mpenzi wake , Rotimi mzaliwa wa Marekani , kwani hiyo ndiyo lugha yake ya mama

Muhtasari

•“Katika safari yangu ya  kusoma Kiswahili, nataka nitembee nanyi. Mimi na mke wangu tumeandika kitabu cha Kiswahili kwa jina Swahili 101” Alisema Rotimi.

Vanessa Mdee na Rotimi
Vanessa Mdee na Rotimi
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki mashuhuri toka Bongo, Vanessa Mdee ameshirikianak na mpenzi wake ambaye ni mwigizaji Olurotimi Akinosho almaarufu kama Rotimi kuandika kitabu cha Kiswahili kwa jina Swahili 101.

Wakizindua kitabu hicho kwenye mtandao wa Instagram, Rotimi ambaye ni mzaliwa wa Marekani kwa wazazi kutoka Nigeria amesema kuwa uandishi wa kitabu hicho ni moja kati ya hatua walizochukua ili ajue kuzungumza Kiswahili.

“Katika safari yangu ya  kusoma Kiswahili, nataka nitembee nanyi. Mimi na mke wangu tumeandika kitabu cha Kiswahili kwa jina Swahili 101” Alisema Rotimi.

Vanessa alisema kuwa amekuwa akitia bidii sana kumfunza Rotimi Kiswahili kwani hiyo ndiyo lugha yake ya mama.

“Kama mnavyojua kuwa mimi nazungumza lugha tatu Kiswahili ikiwa lugha yangu ya mama, tumejifunza kutokana na uzoefu kuwa njia rahisi sana na inayofanya kazi katika kujifunza lugha ni kuitumia katika harakati zote za kila siku maishani” Mdee alisema.

Wawili hao walitaja haswa kupenda sana maneno kama ‘Asante’, ‘Nakupenda’ na ‘Mama Yangu’.

Rotimi aliagiza mashabiki wake kununua kitabu hicho kwani hio ni njia ya kusaidia bara Afrika.