Akothee anafikiria kubadilisha mtindo wake wa mavazi

Mwanamuziki Esther Akoth amesema kuwa nguo refu zake Mama Dorothy Nyong'o zimempendeza na kumtia msukumo kubadilisha mavazi yake

Muhtasari

•Bibi ya gavana Nyong'o alishinda tuzo la WOMA siku za Jumamosi

•Mama Dorothy ni mamake mwigizaji Lupita Nyong'o

Akothee na Mama Dorothy Nyong'o
Akothee na Mama Dorothy Nyong'o
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu kama Akothee amemwandikia Mama Dorothy Nyong’o ambaye ni mke wake gavana wa Kisumu ujumbe maalum akimpongeza kwa kushinda tuzo la WOMA.

Akothee amesema kuwa Mama Dorothy amekuwa msukumo mkubwa kwake na kuwa amemfunza kutulia na kuacha vita zisizofaa.

Mungu atakupeleka kwa mikono ambayo hukujua iko, Mungu atakupeleka kwa nyoyo  ambazo hukujua ziko. Alafu kutakuwa na mama yako mzazi na mama mwingine wa kipekee ambaye Mungu atakutumia Mama, umekuwa msukumo mkubwa sana kwangu tangu nikuone na umenifunza mengi” Akothee aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanamuziki huyo mzaliwa wa Kaunti ya migori amesema  kuwa mtindo wa mavazi wake mama Dorothy umebadilisha mawazo yake

“Hazungumzii mavazi yangu , labda kwa sababu amesafiri sana, lakini nafikiria nafaa kubadilisha  kwa kuwa nimependezwa na mavazi yake refu.” Alisema Akothee.

Alikiri kuwa Mama Dorothy na ambaye ni mama mzazi wa mwigizaji Lupita Nyong’o amebadilisha maisha yake kuwa mema.

Siku ya Jumapili, Gavana Anyan’g Nyong’o alitangaza kuwa Mama Dorothy alikuwa ameshinda tuzo la kimataifa la WOMA(Woman of Magnitude Awards)  kwa jukumu lake kuwapa motisha na kuwawezesha wanawake.

Gavana huyo alimpongeza Mama Dorothy kwa kushinda tuzo hilo linapatianwa mjini NewYork kuwatuza wanawake wanaoshikilia wanawake kwenye jamii.