Nafikiri nimeanza kuzoea maumivu-Msanii Nyota Ndogo akiri

Muhtasari
  • Msanii Nyota Ndogo asema ameanza kuzoea maumivu

Msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo yuko kwenye maumivu baada ya mumewe kuamuacha, baada ya utani wa fools day mwaka huu.

Kulingana na ujumbe wake wa awali msanii huyo yuko tayari kukubali kwamba mumewe amemuacha, na ameanza kuzoea maumivu.

Wawili hao walikuwa katia ndoa yao kwa miaka saba, msanii huyo alimtania mumewe kwamba ana ujauzito, jambo ambalo liliona mumewe kughabika na kumuacha.

"I think nimeanza kuzoea maumivu. Yani namaanisha nikama nimeanza kukubali vile. But siko sure but naona kama na endelea vizuri," Aliandika Nyota.

Awali aiwa kwenye mahojiano msanii huyo alidai kwamba hadhani kwamba mumewe alikuwa anangoja au kutafuta sababu yeyote ya kumuacha.

Pia aifichua kuwa ameekuwa akizungumza na kifungua mimba wa mumewe.