logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Xtian Dela alalamika kupokea jumbe za chuki kutokana na msimamo wake kuhusiana na LGBT

Siku ya Jumapili Dela alikuwa amewahimiza wanajamii ya LGBT kubadilisha maeneo yao ya upigaji kura wahamie Westlands ili wamsaidie kunyakua kiti cha ubunge huku akiwaahidi kutetea haki zao bungeni akichaguliwa.

image
na Radio Jambo

Habari01 June 2021 - 20:26

Muhtasari


•Mwanablogu huyo ambaye ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais miaka ya usoni alikiri kuwa pia yeye ako na marafiki wengi wa jamii ya LGBT na akasihi Wakenya kuwachukulia kwa usawa.

•Dela alitangaza kuwa jumbe alizokuwa anapokea zilikuwa nyingi kiasi kuwa alishindwa kabisa kulala.

Xtian Dela

Mwanablogu Aurther Mandela almaarufu kama Xtian Dela amelalamika kupokea jumbe za chuki kutoka kwa Wakenya kutokana na msimamo wake kuhusiana na mashoga, wasagaji, wanaovutiwa kimapenzi na jinsia za kiume na kike na watu wenye sehemu za siri za kiume na kike pamoja almaarufu kama LGBT.

Kupitia mtandao wa Twitter siku ya jumanne, Dela alitangaza kuwa jumbe alizokuwa anapokea zilikuwa nyingi kiasi kuwa alishindwa kabisa kulala.

"Nimekuwa nikipokea maoni ya chuki, kupigiwa simu, barua pepe na nakala za chuki siku nzima kutokana na msimamo wangu kuhusiana na LGBT. Matusi, chuki na machungu yale ni mengi sana kiasi kwamba sijaweza kulala. Uonevu wa kimitandao ninaopokea umekithiri. Chuki kubwa sana kwa jamii ya LGBT." Dela aliandika.

Siku ya Jumapili Dela alikuwa amewahimiza wanajamii ya LGBT kubadilisha maeneo yao ya upigaji kura wahamie eneo bunge la Westlands ili wamsaidie kunyakua kiti cha ubunge eneo hilo huku akiwaahidi kutetea haki zao bungeni akichaguliwa.

"Ni wakati sisi kama Wakenya tukubali kuwa kuna watu wengi sana wa jamii ya LGBTQI nchini na tupitishe sheria za kuwalinda badala ya kuwasuta na kuwatusi. Mimi mwenyewe sina shida nao mbona tusiwalinde hadharani na kisheria?" aliandika Dela kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanablogu huyo ambaye ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais miaka ya usoni alikiri kuwa pia yeye ako na marafiki wengi wa jamii ya LGBT na akasihi Wakenya kuwachukulia kwa usawa.

"Watu wanafaa kuwa huru kupenda yeyote ambaye wanataka kupenda kibinafsi ama hadharani! Mapenzi ni mapenzi ni wakati Kenya ikubali hilo" Dela alisistiza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved