HONGERA ZARI HASSAN

Zari Hassan ateuliwa kuwa balozi wa Utalii nchini Tanzania

Mwanasoshalaiti huyo ambaye ana watoto wawili na Diamond Platnumz ametangaza kuwa bunge la Tanzania limemtambulisha kama balozi wa hiyari wa utalii

Muhtasari

•Mzaliwa huyo wa Uganda ameeleza mapenzi yake kwa nchi hiyo ambako alikuwa ameoleka kwa kipindi cha miaka nne.

•Zari ambaye kwa sasa anaishi nchi ya Afrika Kusini aliwasiri Tanzania mapema wiki hii kwa huduma za hisani huku wengi wakikisia kwamba alikuwa amefika kumtembelea baba ya wanawe wawili, Diamond Platnumz.

ZARI HASSAN KWENYE SHEREHE YA HISANI
ZARI HASSAN KWENYE SHEREHE YA HISANI
Image: HISANI

Mwanasoshalaiti na mwanabiashara Zari Hassan ni mwanamke mwenye bashasha si haba baada ya kuteuliwa kama balozi wa hiyari wa utalii nchini Tanzania.

Akitangaza uteuzi huo kupitia mtandao wa Instagram siku ya Jumamosi, mwanasoshalaiti huyo ambaye alikuwa mpenzi wake Diamond kwa kipindi cha miaka minne amesema kuwa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limemtambulisha kama balozi hiyari wa utalii nchini humo

.

"Leo nimepata nafasi yenye thamani kwa kuhudhuria mkutano wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo nimetambulishwa kama balozi wa hiyari wa utalii. Ninafurahia kufanya jambo kubwa nilalopenda kuliona likileta matokeo makubwa ili kujenga Uchumi wa Afrika na leo niko Tanzania" Zari aliandika.

Mzaliwa huyo wa Uganda na mama ya watoto watano amekiri mapenzi yake kwa nchi hiyo ambako alikuwa ameolewa kwa kipindi cha miaka nne.

"Tanzania ni sehemu yangu pia, nikivuta hewa na kukanyaga ardhi yake ndani yangu naona msukumo wa kufanya jambo zaidi" alisema Zari.

Ameendelea kuwashukuru wabunge wote, wizara ya maliasili na utamaduni na naibu spika wa bunge la Tanzania, Dr Tulia Akson kwa kumpa wajibu huo.

Zari ambaye kwa sasa anaishi nchi ya Afrika Kusini aliwasiri Tanzania mapema wiki hii kwa huduma za hisani huku wengi wakikisia kwamba alikuwa amefika kumtembelea baba ya wanawe wawili, Diamond Platnumz.