Je Zari Hassan alienda nchini Tanzania kufanya nini?soma uhondo wote

Muhtasari
  • Zari awasili Tanzania kwa ziara ya kutoa msaada
  • KIla mmoja alitoa hisia tofauti, huku asilimia kubwa na wanamitandao wakisema kwamba ameenda kumuona Diamond
  • Zari Hassan na wanawe Tiffah na Nillan wamo Tanzania kwa hafla ya kuwasaidia wasichana na sodo
Zari Hassan

Mitandao ya kijamii imeweka motto baada ya wanamitandao kugundua kwamba mwanasosholaiti wa Uganda na mama wa wanawe staa wa bongo Diamond aliwasili nchini Tanzania siku ya JUmanne.

KIla mmoja alitoa hisia tofauti, huku asilimia kubwa na wanamitandao wakisema kwamba ameenda kumuona Diamond.

Haya yanajiri baada ya miezi miwili, baada ya Diamond kuwa Afrika Kusini amabpo alionekana akiwa na wakati mzuri na wanawe.

Pia kuna wale walisema kwamba Zari atarudiana na Diamond na kumuacha mpenzi wake.

Akiwakwenye mahojiano na Wasafi Zari aliweka wazi kwamba wakati staa huyo alipokuwa Afrika Kusini hakuwa analala nyumbani kwake.

Zari Hassan na wanawe Tiffah na Nillan wamo Tanzania kwa hafla ya kuwasaidia wasichana na sodo..

KUlingana na mama huyo wa watoto 5 alisema kwamba atatembelea shule kadhaa na kuwapa msaada wa sodo.

Dakika chache baada ya uwasili walionekana nyumbani kwake Diamond ambapo alisema kwamba siku ya Jumatano ataembelea shule ya Zanaki na timu yake ya Softcare.

Siku chache zilizopita kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Zari aliandika ujumbe huu;

“Wakwe zangu wa Tandale mpooo😋😋 ilala, Mbagala Temeke Yaan dar nzima bila kuwasahau mashost zangu wa Buza kwa kulengeee alafu namalizia kwa MPALANGE 👌👌👌👌 Nimewamisije sasa👯😊😊 Team nzima ya SoftCare tunajambo letu, guys are u ready ? Mtoto wa kike kujiamini weee👌#Softcare sanitary pad! hivi softcare yenyewe inasemaje !!Mimi nasema.... Do le mi go...folevaaaaaa #softcare See you soon Tanzania 🇹🇿 😍," Aliandika Zari.

Kwa wale sasa ambao walikuwa wanasema kuwa Zari ameenda kumuona Diamond, basi ni wazi kuwa ameanda Tanzania kw ajili ya biashara, na kutoa msaada kwa wasichana.