logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati mwenye bahati! Mwanamuziki atia saini mkataba wa mamilioni ya pesa

Bahati na mkewe Diana Marua wamefanywa mabalozi wa kampuni ya Safaris na kutia saini mkataba wa mamilioni ya pesa

image
na Radio Jambo

Makala23 June 2021 - 05:54

Muhtasari


•"Ushindi mwingine, Bahatis wametia saini mkataba wa mamilioni kuwa mabalozi rasmi wa kampuni  nambari moja ya usafiri, Zunguka Africa Safaris" Bahati aliandika.

•Bahati alizindua albamu mpya mnamo Juni 14 na kufikia sasa amewachilia nyimbo mbili kati ya kumi ambazo ziko katika albamu hiyo. Nyimbo hizo zimeendelea kupokewa vyema na Wakenya

Bahati atia saini mkataba wa mamilioni

Baada ya kuzindua albamu yake mpya 'Love like this' siku chache zilizopita, nyota ya bahati na familia yake imeendelea kung'aa. 

Bahati na mkewe, Diana Marua walifanywa mabalozi rasmi wa kampuni moja ya Zunguka Afrika Safaris na kutia saini mkataba wa mamilioni ya pesa na kampuni hiyo siku ya Jumanne.

Wawili hao walifanya tangazo hilo kupitia mtandao wa Instagram na kupakia picha za hafla hiyo.

"Ushindi mwingine, Bahatis wametia saini mkataba wa mamilioni kuwa mabalozi rasmi wa kampuni  nambari moja ya usafiri, Zunguka Africa Safaris" Bahati aliandika.

Ingawa hakutaja kiwango cha pesa ambacho watakuwa wanapokea kutokana na mkataba huo, mwanamuziki huyo alijivunia kuwa kampuni hiyo iliweza kuwagharamia.

"Hatimaye kampuni ya usafiri ambayo inaweza tumudu" aliandika Bahati.

Bahati alizindua albamu mpya mnamo Juni 14 na kufikia sasa amewachilia nyimbo mbili kati ya kumi ambazo ziko katika albamu hiyo.

Nyimbo hizo zimeendelea kupokewa vyema na Wakenya huku wimbo 'Pete yangu' ambao aliwachilia wiki iliyopita ukifikisha watazamaji zaidi ya  1.4M  nacho kibao 'Take it slow' alichoachilia  Jumatatu kikiwa kimetazamwa na watu zadi ya 467,000 kufikia Jumatano

Mashabiki wameendelea kupongeza Bahati kutokana na ushindi anaoendelea kupata.

Kwa sasa wawili hao wako nchini Tanzania kwa ziara ya kurekodi video ya wimbo 'Kiss' ambao ameshirikisha mwanamuziki wa bongo, Rayvanny.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved