logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Simjui! Jalang'o akanusha madai kuwa mtoto aliye kwenye picha inayoenezwa mitandaoni ni wake

Alieleza kuwa hana uhusiano wowote na mtoto huyo na hana habari zozote kuhusu wazazi wake.

image
na Radio Jambo

Habari23 June 2021 - 07:04

Muhtasari


•Fununu zimekuwa zikitanda kuwa mtoto yule ambaye ana sura kama yake amekuwa akitafuta babake mzazi.

•Alikashifu mwenye kusambaza picha hiyo na kusema kuwa huo ni mzaha ambao huna ladha  kwani alikuwa na nia ya kusambaratisha ndoa yake na ya wazazi wa mtoto yule.

Jalango

Mtangazaji wa tesheni ya Kiss 100, Felix Odiwour almaarufu kama Jalango amekanusha madai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa mtoto ambaye picha yake imekuwa ikienea sana mitandaoni.

Fununu zimekuwa zikitanda kuwa mtoto yule ambaye ana sura kama yake amekuwa akitafuta babake mzazi.

Alipokuwa anazungumzia jambo hilo katika kipindi cha breakfast show, Jalang'o alikanusha uhusiano wowote na mtoto huyo na kueleza masikitiko yake kuhusiana na madai hayo.

"Watu wamekuwa wakisambaza picha ya mtoto huyo na kila mtu ananitaja wakisema kuwa tunafanana" Jalango alisema.

Alieleza kuwa hana uhusiano wowote na mtoto huyo na hana habari zozote kuhusu wazazi wake.

Alikashifu mwenye kusambaza picha hiyo na kusema kuwa huo ni mzaha ambao huna ladha  kwani alikuwa na nia ya kusambaratisha ndoa yake na ya wazazi wa mtoto yule.

"Hebu fikiria kama mkeo hangekuwa mwema kama alivyo na mwenye busara na mawazo mazuri kama alivyo. Kama angekuwa mwenye hasira, angeanza ugomvi" Kamene Goro aliambia Jalas.

Jalango alisema kuwa fununu hizo zingefanya baba ya mtoto yule kutilia shaka  kuwa ndiye baba mzazi wa mtoto.

"Hebu fikiria kama huyo angekuwa mtoto wako ambaye picha yake inaenezwa hivo ikisemekana kuwa ni mtoto wa mtu mwingine? Unapata ninachomaanisha, mambo yanaweza haribika sana" Jalang'o alisema.

Alisema kuwa kuna baadhi ya watu walimshauri apakie picha hiyo kama mzaha tu lakini akawaarifu kuwa kitendo hicho kingekuwa kibaya kwani si mtoto wake. Alisema kuwa jambo hilo lingesababisha hali ya shaka katika familia husika.

(Mtafsiri: Samuel Maina)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved