logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Burna Boy ashinda tuzo la BET; Diamond aibuka wa tatu

Kwa sasa Burna Boy ameshinda tuzo mara  tatu mtawalia.

image
na Radio Jambo

Habari28 June 2021 - 06:59

Muhtasari


•Burna Boy alipata ushindi huo baada ya kuwashinda nyota wengine ulimwenguni kama Aya Nakamura wa Ufaransa, Diamond Platnumz wa Tanzania, Emicida wa Brazil, Headie One(UK) , Wizkid wa Nigeria,Young T & Bugsey (UK) na Youssopha kutoka Ufaransa.

•Kwa upande mwingine, Diamond ambaye aliibuka wa tatu aliwashukuru Watanzania kwa upendo na kumuunga mkono. Alieleza matumaini yake kuwa atapata ushindi wakati mwingine.

Burna Boy na Diamond

Mwanamuziki Burna Boy kutoka Nigeria ameshinda tuzo la Best International Act katika hafla ya BET Awards 2021.

Burna Boy alipata ushindi huo baada ya kuwashinda nyota wengine ulimwenguni kama Aya Nakamura wa Ufaransa, Diamond Platnumz wa Tanzania, Emicida wa Brazil, Headie One(UK) , Wizkid wa Nigeria,Young T & Bugsey (UK) na Youssopha kutoka Ufaransa.

Mwanamuziki huyo tajika barani Afrika na kote duniani sasa ameshinda tuzo kwa mara ya tatu mtawalia.

Akipokea tuzo hilo, Burna Boy ambaye alionekana  kujawa na bashasha  alijivunia ushindi wake wa tatu kuahidi kuwa ataendelea kutia bidii kwenye taaluma yake ya muziki.

"Ushindi wa tatu mtawalia, mnanipata? Hakuna kusimama. Nawapenda sana BET" Burna Boy alisema.

Kwa upande mwingine, Diamond ambaye aliibuka wa tatu aliwashukuru Watanzania kwa upendo na kumuunga mkono. Alieleza matumaini yake kuwa atapata ushindi wakati mwingine.

Hata hivyo, Diamond alikuwa amekumbana na pingamizi kubwa kutoka kwa raia wa Tanzania ambao hawakupendezwa na kuteuliwa kwake. Baadhi yao walitaka jina lake kuondolewa kwenye orodha ya wasanii waliokuwa wameteuliwa kupokea tuzo


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved